HEBU TUPIA MACHO JINSI LULU ALIPOENDA KUMPA POLE WASTARA, HUZUNI YATAWALA


 

 

MWISHONI mwa wiki iliyopita, msanii Elizabeth Michael “Lulu” alikwenda kumpa pole msanii mwenzake Wastara Juma kwa kufiwa na mumewe, Sajuki…
 
 
 
 
Huzuni ilitawala nyumbani kwa Wastara mara baada ya Lulu kuwasili, lakini hatimaye baada ya muda mrefu wa maongezi nyuso za wasanii hao zikapambwa na tabasamu.Wameandika jamaa wa http://www.saluti5.com

SUMA-LEE AELEZA KILICHOFANYA ASIJE KUMZIKA BABA YAKE ….ALAUMU WAFANYAKAZI WA UBALOZI WA TANZANIA UK


 

 


MSANII SUMALEE

Taarifa za msiba wa baba yake mzazi alizipata alhamisi iliyopita akiwa bado yuko nchini Uingereza ambako alikwenda kufanya show toka december 2012.

Baada ya kupata taarifa ilibidi afanye utaratibu wa kupanga safari kurudi nyumbani ili amzike baba yake lakini wakati huohuo siku chache nyuma alikua amepeleka hati yake ya kusafiria Home Office ili aongezewe muda wa miezi mitatu kuendelea kukaa Uuingereza ambako alipata dili pia alikua na mipango ya kufanya video mpya kabla ya kurudi home.

Alishughulikia ticket mchana huohuo alipopata taarifa na akafanikiwa ila tatizo likawa ni kupata documents za kusafiria ili awahi kuja kumzika baba yake siku inayofata ambayo ni ijumaa.

Namkariri Sumalee akisema “niliambiwa we kata ticket ila documents za kusafiria tutapiga simu mtu aende kuchukua ubalozi wa Tanzania U.K ila kuna jamaa pale ubalozini anaitwa Sylvester Ambukile nikaongea nae kwenye simu nikajitambulisha nikamwambia nimefiwa naomba travel documents nikazike, hakutaka kunielewa kabisa yani ndio kwanza ananiambia hatuwezi kukupa kithibitisho kwa sababu passport yako ipo sio kwamba imepotea, wakati huo ilikua ni saa nane mchana na ndege niliyokata ticket inaondoka saa moja usiku”

“Tumewapigia wenzake ubalozini ndio wakaniambia huyu huyo ndio anahusika, dakika za mwisho mwisho ndio tukampata balozi wa Tanzania U.K akasema mbona hiyo inawezekana ila haiwezekani kutoa travel documents bila kupata jina la mtu kuulizia kule home office kama jina lako lipo kweli manake kuna wengine wanafanya makosa wanatafutwa na askari wanataka document ili wakimbie nchi lakini wewe ulitakiwa kumkabidhi jina lako ili aulizie home Office, wakati huo muda ulikua umepita tayari ilikua saa kumi na mbili na nusu ofisi zimeshafungwa” – Sumalee

Mbali na hayo Sumalee amesema “ningefanikiwa kusafiri Alhamisi ningewahi kuzika kabisa lakini kibinaadamu huyu jamaa Sylvester Ambukile nitamlaumu mpaka kufa kwa sababu siwezi kusahau hili tukio kwa sababu ni kitu ambacho kilikua kinawezekana, na sio mimi tu amepigiwa na watu hata 15 wa hapa London kila mtu anamwambia swala langu lakini jamaa alikua anasema siwezi, sitaki na sitaweza, hataki kuelezea hataki kufanya chochote”

HOJA BINAFSI YA MNYIKA KUHUSU KUPATIKANA KWA MAJI SAFI


 
MAELEZO NA HOJA BINAFSI YA KUPENDEKEZA BUNGE LIJADILI NA KUPITISHA MAAZIMIO YA HATUA ZA HARAKA ZA KUBORESHA UPATIKANAJI WA MAJI SAFI NA USHUGHULIKIAJI WA MAJI TAKA KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM KWA MUJIBU WA KANUNI YA 54 FASILI YA (1) YA KANUNI ZA KUDUMU ZA BUNGE TOLEO LA MWAKA 2007
 
John John Mnyika
Mheshimiwa Spika;
Awali ya yote niungane na wote wenye mapenzi mapema katika kuomba ulinzi wa Mwenyezi Mungu wakati tukitimiza wajibu wa kibunge kwa mujibu wa ibara ya 63 ya Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania wa kuwawakilisha wananchi, kuisimamia serikali, kuidhinisha mipango na kutunga sheria.
 
Mheshimiwa Spika;
Aidha, kwa namna ya pekee ni kushukuru wewe binafsi na uongozi mzima wa Bunge kwa kunipa fursa hii adimu na adhimu ya kuwasilisha hoja binafsi kwa mujibu wa kanuni ya 54 fasili ya (1) ya kupendekeza bunge lijadili na kupitisha maazimio ya hatua za haraka zaidi za kuboresha upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka katika Jiji la Dar es salaam.
 
Mheshimiwa Spika;
Maji ni uhai, hivyo matatizo ya upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka katika Jiji la Dar es salaam na nchini kwa ujumla kama hatua za haraka zisipochukuliwa yatageuka kuwa janga la taifa. Katika kila watanzania katika Jiji la Dar es Salaam na nchini; kwa wastani mmoja hapati huduma ya maji safi na salama na hali ni mbaya zaidi kuhusu ushughulikiaji wa maji taka.
 
Wakati baadhi ya nchi duniani zikielezwa kwenye kitabu cha hivi karibuni cha Mnukuzi Maalum wa Umoja wa Mataifa (UN Special Rapporteur) kuwa katika mwelekeo unaostahili kuhusu kuhakikisha haki ya maji na usafi wa mazingira (On the right track; Good practices in realizing the rights to water and sanitation: 2012), hali ni kinyume kwa taifa letu.
 
Ripoti ya Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia masuala ya maji (WaterAid: 2011) imeiweka Tanzania katika kundi la nchi ambazo haziko katika mwelekeo unaostahili wa kuboresha upatikanaji wa maji safi, ushughulikiaji wa maji taka na usafi wa mazingira (Policy Report: Off Track, Off Target; why investments in water, sanitation and hygiene is not reaching those who need the most).