WEMA AJINUNULIA MASHINE YA MASAJI, JENEZA LA JIDE


WOSIA KIFO CHA JIDE

 

Na Mwandishi Wetu

TAKRIBAN mwaka mmoja tangu alipoeleza aina ya jeneza atakalotaka azikwe siku akifa, mwanamuziki  Judith Wambura ‘Jide’ au ‘Anaconda’  ameibua jingine jipya, safari hii ameandika wosia wa kifo chake, Ijumaa lina uchambuzi kamili.

Judith Wambura ‘Jide’.

ATIMIZA AHADI

Kama alivyoahidi mashabiki wake wiki moja iliyopita kupitia mtandao wake wa kijamii, Jumatano ya Mei Mosi, mwaka huu, mishale ya saa 8:00 mchana, Jide au Komando aliandika wosia huo wenye maneno 555 akiwataja watu ambao asingetaka wafike kwenye msiba wake siku…

Na Mwandishi Wetu
TAKRIBAN mwaka mmoja tangu alipoeleza aina ya jeneza atakalotaka azikwe siku akifa, mwanamuziki  Judith Wambura ‘Jide’ au ‘Anaconda’  ameibua jingine jipya, safari hii ameandika wosia wa kifo chake, Ijumaa lina uchambuzi kamili.

Judith Wambura ‘Jide’.

ATIMIZA AHADI
Kama alivyoahidi mashabiki wake wiki moja iliyopita kupitia mtandao wake wa kijamii, Jumatano ya Mei Mosi, mwaka huu, mishale ya saa 8:00 mchana, Jide au Komando aliandika wosia huo wenye maneno 555 akiwataja watu ambao asingetaka wafike kwenye msiba wake siku akifariki dunia.

NI KWA WATANZANIA WOTE
Katika sentensi nyingine, mwanadada huyo ameandika wosia huo kwa Watanzania wote watakaokuwa bado hawajatangulia mbele ya haki yeye atakapofikwa na mauti.

ASIOTAKA WAFIKE
Katika wosia huo, Jide alitupa tuhuma nzito kwa mabosi wa Clouds Media Group hasa Radio Clouds FM, Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba kuhusika katika kumhujumu kwenye tasnia ya muziki nchini huku akiwataka wasifike kuaga maiti yake.

RADIO ISITANGAZE KIFO CHAKE
Katika kuupitia wosia huo, Ijumaa limebaini kuwa, Jide alizuia Kituo cha Radio Clouds FM kisitangaze kifo chake wala kupiga nyimbo zake siku atakapokufa.

AJITOA FIESTA, KISA?
Ndani ya wosia huo, mwanamuziki huyo aliendelea kudai kuwa alijitoa kwenye shoo za Fiesta zinazofanyika kila mwaka ambapo kwa mara ya mwisho alilipwa Sh. 800,000 na kuanzia hapo ndipo fukuto la kubaniwa lilipoanza.
Alisema bifu likapamba moto mwaka 2003 alipotoa albamu yake ya pili iliyojulikana kwa jina la Binti.

KISA? MACHOZI BAND
Aliandika kuwa tatizo lingine lililochochea yeye kukandamizwa ni baada ya kuacha kufanya shoo za Clouds na kuanzisha bendi yake ya Machozi ambapo alijiajiri mwenyewe na kupata mafanikio jambo ambalo anadai jamaa hao hawakulipenda hivyo kuanza kuchochea mbinu za ‘kumuua’ kisanii.

KUKANDAMIZWA
Aliwatuhumu kuwa kwa muda mrefu ‘wabaya’ wake hao wamekuwa wakifanya njama za kumkandamiza ili kuhakikisha anapotea kabisa kwenye muziki.

ASISHIRIKIANE NA WASANII WENGINE?
Alizidi kuandika kwamba watu hao wamekuwa wakitishia kutopiga nyimbo zake alizoshirikishwa na wasanii wengine wa Bongo.

FITINA
Jide aliandika: Nilinyamaza kwa muda mrefu lakini kadIri muda ulivyosonga mbele ndivyo hali ilivyozidi kuwa mbaya kwani jamaa hao waliongeza fitina kwangu kila kukicha.

VIKAO VINNE
Jide aliendelea kutuhumu kuwa jamaa hao hadi sasa walishakaa vikao vinne vilivyolenga kumpoteza kabisa kwenye ramani ya muziki huku akidai ni wafitini ambao wamekuwa wakipita kila mahali kuhakikisha wanaziba mrija wa kumuingizia ‘chochote kitu’.

UPANDE WA PILI UNASEMAJE?
Baada ya kuutathimini wosia huo na kuona ni kwa jinsi gani ulivyojaa tuhuma zilizohitaji majibu, kama kawaida ya Ijumaa lililojaa weledi lilitafuta upande wa pili, Clouds Media Group ili kupata majibu ya kile alichokiandika msanii huyo.
Mmoja wa mabosi wa Clouds ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini  kwa kuwa si msemaji wa kampuni, pamoja na kukiri kuuona wosia huo, alichambua kipengele kimoja baada ya kingine.

KUHUSU KUBANIWA
“Kama ana ushahidi ni lini alibaniwa aweke data mezani. Unajua watu wametengeneza kizazi cha chuki bila kuwa na sababu ya msingi.
“Hata msanii chipukizi akiibuka leo ataambiwa fulani anabaniwa na kujikuta akijenga chuki bila kujua anayeeneza hayo ana lengo gani.
“Ipo mifano ya wasanii wengi ambao nyimbo zao hazipigwi katika vituo f’lanif’lani vya redio (akavitaja) kama Diamond na Juma Nature, mbona huko hawapaoni wanaona Clouds pekee?”

KUHUSU KUKANDAMIZWA
“Kama kuna ushahidi ni lini aliandaa shoo au aliitwa kwenye shoo then (halafu) watu wakamkandamiza kwenye malipo auweke wazi, kwani hakuna mikataba? Ingekuwa ni vizuri akatoa mikataba kuwa alikandamizwa kuliko kujenga chuki zisizokuwa na msingi. Anasema alilipwa shilingi laki nane, kwa nini hakukataa? Kwani alilazimishwa?”

KUHUSU ASISHIRIKIANE NA WENZAKE
“Ukweli ni kwamba hatujawahi kubana kupiga wimbo wa mtu kisa ameshirikishwa yeye. Hayo ni maneno ambayo mwisho wa siku hawezi kuthibitisha kwa data.”

KUHUSU KUMFITINI
“Mtu amfitini ili apate faida gani? Kama hakuna faida hakuna sababu ya kumfitini mtu katika biashara yake.”

VIKAO VINNE NA KIFO
“Hayo mengine ya vikao mimi siyajui na siwezi kuzungumzia kifo cha mtu kwani huo ni wosia wake.”

KUNA KITU KIKUBWA KINAKUJA
Kwa mujibu wa bosi huyo, hali inavyoendelea kuna kitu kikubwa kinakuja na ili kuweka sawa mambo haya, Clouds wataitisha mkutano mkubwa wa waandishi wa habari ili kuifahamisha jamii ni nini hasa kinaendelea.
Baada ya bosi huyo kutoa ufafanuzi juu ya tuhuma za msanii huyo, Ijumaa lilimtafuta meneja wake Jide, Gardner G. Habash ili aweke wazi kama tuhuma alizotoa mwanamuziki huyo zina ushahidi wa kushika, lakini bila mafanikio.

JIDE KATIKA SIKU ZA KARIBUNI
Katika siku za hivi karibuni, Jide amekuwa akitumia mitandao ya kijamii kueleza jinsi anavyoandamwa na kituo hicho cha redio na kusababisha kuibuka kwa mijadala mbalimbali kutoka kwa wasomaji wake.Chanzo:www.globalpublishers.info

 

HOTUBA ya Kambi ya Upinzani iliyosomwa na Lissu, Katiba na Sheria, yaibua makubwa bungeni


Image

 
MAONI YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI, WIZARA YA KATIBA NA SHERIA,
 
MHESHIMIWA TUNDU A.M. LISSU (MB.)
KUHUSU
MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA KWA MWAKA 2013/2014
 
(Kanuni ya 99(9) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2013)
 
UTANGULIZI
 
Mheshimiwa Spika,
 
Ofisi ya Waziri wa Katiba na Sheria imeanzishwa kwa mujibu wa kipengele cha 12 cha Nyongeza ya Waraka wa Rais uliochapishwa kama Tangazo la Serikali Na. 494 la tarehe 17 Desemba 2010. Majukumu ya Ofisi hii yameainishwa katika Tangazo la Ukasimishaji wa Majukumu ya Kiuwaziri la mwaka 2010 (The Ministers [Assignment of Ministerial Functions] Notice, 2010) lililochapishwa katika Gazeti la Serikali kama Tangazo la Serikali Na. 494A la tarehe 17 Desemba 2010. 
 
Kwa mujibu wa Nyongeza ya Pili ya Tangazo hilo, pamoja na mengine, Ofisi ya Waziri wa Katiba na Sheria imekasimiwa majukumu ya masuala ya kikatiba, uendeshaji na utoaji wa haki, uendeshaji mashtaka na haki za binadamu. 
 

Kwa sababu ya matukio ya hivi karibuni yanayohusu utendaji wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mchakato wa Katiba Mpya na kwa kuzingatia umuhimu wake katika mustakbala wa taifa letu, tunaomba kuanza na masuala yanayoihusu Tume na uendeshaji wake wa mchakato huo.
 

Beaking Newssss: Mtu Mmoja ajulikanae kwa Jina la Shirima mfanyabiashara wa Kariakoo amejitupa kutoka Gorofa ya 9 muda huu.


 

 

 

Pichani ni mfanyabishara aliyetambulika kwa jina la Shirima aliyejirusha  kutoka Ghorofa ya 9 katika hoteli ya  Concord Kariakoo jijini Dar na kuangukia kwenye TAXI iliyokuwa imepaki chini ya Hoteli hiyo. Chanzo cha mkasa huo bado hakijulikani nini kilichomsibu mfanyabiashara huyo  ambapo mwili wake umekimbizwa Hospitali. Chanzo cha habari hizi kinaendelea kufuatilia kwa undani zaidi na kutujulisha hapo baadae. Source:  bofya hapa

Mitihani Kidato cha Nne kusahihishwa Upya


 

wpid-Prime-Minister-Mizengo-PindaWaziri Mkuu Mizengo Pinda aliyeunda tume ya kuchunguza kufeli kwa wanafunzi wengi mwaka 2012.

………………………………………………………..

Tume ilioundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuchunguza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana, LEO imeitaka serikali ifute matokeo yote na mitihani isahihishwe upya.

Akisoma ripoti ya Tume hiyo hivi punde bungeni Mjini Dodoma, Waziri wa Nchi Katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia sera na uratibu, William Lukuvi amesema kwamba mitihani hiyo inapaswa kusahihishiwa kwa kuzingatia vigezo vilivyotumika katika kusahihisha mitihani ya kidato cha nne mwaka 2011.

Mwaka jana matokeo ya wanafunzi wa kidato cha nne yalikuwa mabaya kuliko matokeo mengine yaliowahi kutolewa na Baraza la Mitihani la Taifa. Wanafunzi walifeli kwa asililimia 60.

Kutokana na matokeo ya tume hiyo, Lukuvi ameipongeza tume hiyo kwa kutoa matokeo hayo.

Wataalamu wa elimu wanasema kwamba endapo serikali itatekeleza pendekezo hilo itaingia kwenye gharama kubwa ambazo pengine zitaigharimu serikali.

Kwa hisani ya Habarimasai.com

WAKATI MWINGINE WANAWAKE HUKOSEA BILA KUJUA!-2


KUKOSEA ni kujifunza. Ukifanya kosa na kutambua, bila shaka huwezi kurudia tena na kama ikitokea hivyo utakuwa umekusudia. Hapa nazungumzia makosa ambayo hufanywa na wanawake bila kujua.

Wiki iliyopita nilieleza baadhi yake, leo nahitimisha katika vipengele vingine. Rafiki zangu, wanaume hawawapendi kabisa wanawake ambao wanawasema vibaya wanawake wenzao.
Hapa kuna aina mbili, kuwateta au kuwaita majina yenye maana mbaya na yanayodhalilisha. Utakuta mwanamke amekaa na mumewe anathubutu kuwaita wenzake majina kama changu, malaya, dadapoa, mhuni, mlupo na mengine yanayofanana na hayo.
Tabia hii haipendezi na unafanya mwanaume wako akufikirie vibaya na inawezekana nawe ni aina ya wale wanawake wenye ‘mdomo’ sana. Tafakari hili.

UZUNGU MWINGI…
Kupenda kumshika kimahaba, kumkumbatia au kuwa naye kimapenzi zaidi mbele za watu, kunamfanya mwenzi wako aone kama umepungukiwa tabia njema. Kwa tafsiri ya haraka, ataona huna staha.
Kujionesha mbele za watu mkifanya mambo yanayoashiria mapenzi, kunawapunguzia heshima na pengine mtaonekana kama wahuni tu na siyo wenzi mnaotumia akili wenye ndoto njema za baadaye.

KIPAUMBELE KUHUSU NGONO
Wanawake wengi wanaharibiwa na hisia kwamba wanaume wapo nao kwa ajili ya mapenzi (ngono) tu! Kwamba, silaha ya mwisho katika mapenzi yao ni kukutana faragha! Hii si kweli.
Wanaume wanapenda wanawake makini, ambao wapo nao kwa ajili ya maisha zaidi. Wanaowaza mambo ya maisha na siyo ngono. Mbaya zaidi, hawapendi kabisa uoneshe kwamba unajua ‘hapindui’ kwako kwa sababu unampatia faragha.
Kumbuka ngono inawezekana kupatikana kwa njia yoyote lakini si amani na mustakabali mzuri wa maisha ya baadaye.

SULUHU YA MIGOGORO
Mwerevu ni yule anayegundua kwamba amekosea halafu anaanza upya kutafuta njia za kutoka kwenye makosa. Huu ndiyo werevu. Siku zote mwanamke mwenye busara na nia njema na uhusiano wake, hapendi kumkosea mpenzi wake na hata kama akifanya hivyo, anakuwa mwepesi sana wa kutafuta njia za kuweka sawa uhusiano wao.
Sifa ya kumaliza migogoro mapema ni bora sana. Wanawake wengine hawaoni kama lina umuhimu mkubwa. Hili ni kosa kubwa.

UMENIPATA RAFIKI?
Mapenzi ni kujifunza na pia unatakiwa kufahamu kwamba hakuna mbabe wala mjinga wa mapenzi. Ukijua kosa lako, utajirekebisha na kuboresha uhusiano wako, wakati ukitafuta elimu zaidi juu ya mapenzi.
Makosa haya usikubali kuyafanya tena, badilika huku ukiendelea kujifunza zaidi. Kuna mjanja kama wewe? Wiki ijayo nitakuwa tena hapa kwa mada nyingine. 

Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Mambo ya Mapenzi anayeandikia Magazeti ya Global Publishers. Ameandika Vitabu vya True Love, Let’s Talk About Love na All About Love vilivyopo mitaani.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, Profesa Mwesiga Beregu, amekataa kata kata wito wa chama chake wa kumtaka ajotoe ndani ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, “TANZANIA NI MUHIMU KULIKO CHADEMA…..SIPO TAYARI KUSUSIA MCHAKATO WA KATIBA”…..HAYA NI MAJIBU YA PROFESA BEREGU KWA DR SLAA


 

 
 
 
 
Raia Mwema:

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha demokrasia na Maendeleo (Chadema), Profesa Mwesiga Beregu, amekataa kata kata wito wa chama chake wa kumtaka ajotoe ndani ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba,huku yeye akiweka msimamo wake wazi kwamba Tanzania ni muhimu zaidi kwake kuliko chama chake hicho.

Habari zilizoppatikana na kuthibitishwa Profesa Baregu, zinasema katibu Mkuu wa chama hicho Dk Wilbroad Slaa, alimwiita msomi ambae ni mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, akimtaka ajitoe. Ndani ya Tume hiyo kwasababu za kisiasa kwa madai kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeuteka mchakato huo.

Profesa Beregu anaelezwa kumjibu Dk Slaa kwa kutumia maneno ya kiingereza, “If I am told to choose between my country and my party (Chadema), I will choose my country”, akiwa na maana kwamba kama angetakiwa kuchagua kimoja kati ya nchi yake na chama chake cha Chadema, angechagua nchi yake kwanza.

Akizungumza na Raia Mwema juzi Jumatatu jijini Dar es Salaam, Profesa Baregu amekiri kutoa msimamo huo Katibu Mkuu wake Dk Slaa, pamoja na chama chake cha Chadema, akisema viongozi wenzake hao wanapaswa kujishauri mara mbili mbili kabla ya kuchukua uamuzi huo wa kujitoa ikizingatiwa. Kwamba tangu mwanzo chama hicho ndicho kilichoasisi suala zima la Tanzania kuwa na Katiba Mpya tofauti na hii ya sasa.

Itakumbukwa kwamba Chadema, kupitia kwa Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, wakati akiwasilisha hotuba mbadala ya kambi rasmi ya upinzani kwa Ofisi ya Waziri mkuu, alitangaza kujitoa katika mchakato wa mabadiliko ya katiba akitaja sababu kadhaa, zikiwamo za mchakato mzima huo kutekwa na CCM na lakini pia kwamba wajumbe wa Tume hiyo hawana weledi wa kutosha kufanya kazi hiyo.

“Ni kweli niliitwa na katibu Mkuu (Dk Slaa), akaniambia Kamati Kuu ya chama chetu imeazimia kwamba chama hakiridhishwi na mchakato mzima wa kutunga Katiba mpya, na kwa hiyo akaniambia chama kimeagiza nijitoe ndani ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Akaniambia Kamati Kuu imeamua mambo mawili; kwanza kijitoe na pili, kikishajitoa kianzishe kampeni ya nchi nzima kuwahamasisha wananchi nao wasusie mchakato huo”anasema Profesa Baregu katika mahojiano maalum na Raia mwema.

Anasema aliomba kujulishwa rasmi maamuzi hayo ya CC kwa maandishi, ili ajue atachukua uamuzi ganilakini hadi anafanya mahojiano na Raia mwema hakuwa amepata majibu huku akisema kwamba kwa maoni yake kama kweli yalikua ni maamuzi ya kikao, basi Kamati Kuu itakuwa ilifanya makosa kufikia uamuzi wa kujitoa bila kumshirikisha.

“Kwanini? Mimi tangu mwanzo kaabisa sikuona kama suala hili la kuandikwa kwa Katiba mpya ni suala la mapambano kwa sababu kubwa moja kwamba Chadema ndiyo mwasisi wa mabadiliko haya ya katiba. Mimi nilikuwa Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2010 na nilishiriki kuandika ilani ya uchaguzi, na hili la kutaka Katiba mpya lilikuwemo ndani ya Ilani yetu.

Wakati ule wenzetu (CCM) waliweka msimamo wao wakisema hakuna sababu ya kuwa na katiba mpya, iliyopo inatosha,lakini baadae Serikali ikaona ipo haja ya kuwa na katiba mpya inayokidhi mahitaji ya sasa na yajayo. Muswada ukapelekwa Bungeni, wabunge wa upinzani wakasusa na kutoka nje. Chadema tukapewa fursa ya kwenda Ikulu kuonana na Rais kwa siku mbili mfululizo na karibu mapendekezo yetu yote yakakubaliwa.”

“Muswada ukarudishwa Bungeni upya, sheria ikafaniwa marekebisho na kukubalika na wabunge wa kambi ya upinzani. Sasa leo hii, wabunge wale wale waliokubali, wanataka kukataa mchakato wa katiba unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria waliyoipitisha wao wenyewe….kwa maoni yangu, hadi sasa sijaona matatizo ya mchakato., yawe ya maandishi au ya malengo ya kisheria. Kama ningekuwa nimeona tatizo nisingekuwa humu, ningejitoa, Tunatengeneza Katiba yetu Watanzania wote, si Katiba ya Chama fulani…

“Lakini pia, chadema tulipokutana na Rais (Jakaya Kikwete), alitushauri na tukakubaliana naye, twende hatua kwa hatu. Itungwe sheria yenyewe kwanza, halafu iundwe tume, baada ya hapo mambo mengine yaendelee kujadiliwa…(Angu wakati huo hadi sasa nadhani sisikama Tumetunafanya vizuri ikilinganishwa na wenzetu wa huko nje walioandika upya Katiba yao.

“Mchakato unaofuata sasa ni wa kuundwa kwa bunge Maalumu la katiba, hatua hii nayo Wananchi wanetakiwa wajiandae kutoa maoni yao juu ua muundo wa. Bunge hilo. Ushauri wangu kwa Chadema., naomba chama chetu kikae mkao wa kujenga nchi yetu, si. Mkao wa kuibomoam Kama Chama tukae na Watanzania kujenga Katiba yetu mpya kwa ajili ya Watanzania na Tanzania yetu hii kwasababu fursa hii haitakuja tena karibuni labda baada ya miaka 50 ijayo….kuzira, kujitoa, nasema Watanzania hawatatuelewa”

Kaifafanua msimamo wake alioutoa kwa Dk Slaa kwamba kama angeambiwa achague kati ya ncchi yake na chama chake, angechagua nchi kwanza, Profesa Baregu anasema “Ndio, chama kinaundwa kinapita, lakini Tanzania kama nchi itaendelea kuwepo daima. Ushauri wangu kwa Chadema ni kwambakwa kuwa sisi tulishajiweka katika kusimamia mchakato wa Katiba mpya, tusijiharibie kwa kuvuruga mchakato huu”

Akizungumzia kauli ya Mbowe katika hotuba yake bungeni kwamba Tume ya Mabadiliko ya Katiba haina watu weledi, Profesa Baregu anasema “Sisemi katika hili Chadema imekurupuka, nasema ijishauri upya, sijui ni weledi wa aina gani wanaousema, lakini naamini Tume yaMabadiliko ya Katiba imejaa watu weledi watupu, imejaa watu waadilifu na wasiokuwa na matope yeyote…,ndiyo maana tangu iundwe, hakuna Mtanzania yeyote ambae ameiita Tume hii kwamba ni genge jingine la mafisadi.

“Sitaki kuwasemea wajumbe wanzangu juu ya weledi wao, lakini mimi mwenyewe tu mbali na elimu yangu, lakini pia nimetumika katika Tume ya Month Ibrahim inayotathimini utawala bora wa marais wa Afrika kwa muhula mmoja, mtu huwezi huwezi kuwa katika tume hiyo kama huna weledi wa kutosha”

Dk Slaa alipotafutwa jana Jumanne,ili pamoja na mambo mengine alezee hatua hiyo ya Profesa Baregu kukataa kujiuzulu akiweka wazi kwamba hadi sasa hajaona tatizo lolote kubwa ndani ya Tume hiyo linaloweza kumshawishi akubaliane na msimamo wa chama chake, na msisitizo wake huo wa kuweka maslahi ya nchi kwanza mbele kuliko chama chake alisema “Saa hizi niko kwenye kikao, pole baba”