BUNGENI FEB 8, DODOMA… MHE. MBATIA KUTAKIWA KUJIUZULU

 

.

Waziri mkuu Mizengo Pinda amelazimika kuingilia kati mjadala wa wabunge kuhusiana na hoja iliyotolewa wakati wa mjadala wa mabadiliko ya sheria mbalimbali kuhusu kutoingiliwa kwa maamuzi yanayotolewa na wazee wa Mahakama kwenye baadhi ya mashauri yanayohusiana na masuala ya dini ya kiislam ikiwemo ndoa na mirathi.

Wakati hoja ikiendelea kabla ya kupitishwa kwake, Waziri mkuu alisema ipo haja ya serikali kuliangalia upya hilo jambo na kutahadharisha kwamba huo mjadala ungeendelea ungeweza kuligawa taifa kwa misingi ya udini ishu ambayo ilisababisha mwanasheria mkuu wa serikali Jaji Frederick Werema kukifuta hicho kifungu.

.

Kwenye sentensi nyingine ni kwamba ishu ya mitaala ya elimu Tanzania iliendelea kumuandama mbunge wa kuteuliwa na rais Kikwete, James Mbatia baada ya mbunge wa Nzega Dk Khamis Kigwangalla kuomba muongozo wa spika kutoa hoja ya bunge kumwajibisha James Mbatia kwa kuongea uongo bungeni.

Namkariri Kigwangalla akisema “utaratibu uliovunjwa kwa mujibu wa kanuni ya 63 ni kusema uongo bungeni, imethibitika bila shaka yoyote kwamba Mh James Mbatia alilidanganya bunge, alilidanganya bunge na kusema atakua tayari kujiuzulu mitaala hiyo ikiletwa”

Mh James Mbatia.

Mh Kigwangalla alimalizia kwa kusema “naomba atumie uungwana yeye mwenyewe kusimama katika bunge hili.. aidha kuwaomba radhi Watanzania kwa kudanganya ama kutimiza wajibu aliousema wa kujiuzulu, uongo aliousema ni mkubwa sana.. naomba nitoe hoja kwamba Mh Mbatia aadhibiwe kwa mujibu wa kanuni ya 63, asihudhurie vikao visivyozidi 20 na aombe radhi kwa maandishi kwa Watanzania kwa kusema uongo bungeni”

Baada ya Mh Kigwangalla kumaliza kuongea Mbunge wa Kasulu mjini Moses Machari alisimama na kusema “Mh Mbatia hakuzungumza uongo kutokana na ushahidi ambao hata mimi ninao, waziri alilitaarifu bunge hili kwamba mitaala ya sasa inayotumika ndani ya nchi yetu ni ya mwaka 2005 na kwa mujibu wa rasimu ya mtaala tuliyonayo sisi inaonyesha iko mitaala miwili ambayo imeandaliwa mwaka 2005 chapa ya kwanza mwaka 2012 jambo ambalo linajustify kwamba baada ya kuulizwa mwaka jana ndio walianza kwenda kutengeneza”

Mh Moses kwenye sentensi nyingine namkariri akisema “ilikua ni swala la kwenda kuchakachua, kupika na hicho kilichowasilishwa ndani ya bunge lako Mh Mwenyekiti hatukua na imani toka mwanzo kwa sababu tunao waraka wa serikali, hatuna imani na hata alichokua anazungumza Mh Kigwangalla kwamba Mh Mbatia amedanganya, kwanza waanze waende wakaadhibiane wao wenyewe”

Kwa kumalizia namkariri mwenyekiti wa bunge Jestina Mhagama akisema “hatuna kifungu ambacho kinawaambia wabunge huyo mbunge sasa ajiuzulu ila mbunge mwenyewe anapotoa kauli ya kujiuzulu, yeye mwenyewe anao uwezo wa kupima je kwa haya yanayojiri yanafanya aendane na kile alichokisema, kwa yaliyotokea nijiuzulu au nisijiuzulu… kwa hiyo iko mikononi mwa mbunge mwenyewe lakini sisi kama Bunge hatuna mamlaka kwa mujibu wa kanuni kumwajibisha huyo mbunge ajiuzulu”

One Comment

Leave a comment