DAKTARI WA MUHIMILI WAANZA MGOMO LEO KUSHINIKIZA KULIPWA POSHO ZAO


DAKTARI WA MUHIMILI WAANZA MGOMO LEO KUSHINIKIZA KULIPWA POSHO ZAO

 Dkt. Frank Kagolo, ambaye ni miongoni mwa madaktari wanaofanya kazi kwa mkataba wa mwaka mmoja katika Hospitali ya Muhimili, akizungumza na waandishi wa habari wakati akihojiwa kuhusu mgomo wao waliouanzisha leo kutokana na kucheleweshewa kulipwa posho zao za mwezi mmoja.
Baadhi ya Madaktari na Mafamasia wanaofanya Kazi kwa Mafunzo kwa mkataba wa mwaka mmoja hospitari ya Taifa Muhimbili wakiwa katika mkutano na viongozi wa Wizara ya Afya na hospitali hiyo Dar es salaam leo baada ya kugoma kwa kutolipwa posho zao kwa muda wa mwezi mmoja.Chanzo:sufianimafotoblog

WAZIRI MAGUFULI ATOA TAARIFA KUHUSU MRADI WA UPANUZI WA BARABARA YA KILWA – AWAMU YA PILI


Waziri wa Ujenzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Magufuli (MB) leo ametoa taarifa ya pamoja na Balozi wa Japan hapa nchini Mh. Masaki Okada iliyohusu Mradi wa Upanuzi wa barabara ya Kilwa kwa Awamu ya pili.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, Mh. Magufuli ameelezea hatua iliyochukuliwa na Wizara yakekwa Pamoja Balozi wa japan ya kuunda Kikosi Kazi cha Pamoja kilichochunguza kuharibika mapema kwa barabara ya Kilwa hasa katika sehemu iliyojengwa katika Awamu ya Pili ya Mradi huo.

Aidha amefafanua kuwa mpango wa Mkandarasi wa kuanza matengenezo ya barabara hiyo ni mwezi Mei 2012 baada ya kipindi cha mvua.

Tamko la wanachama wa cuf dar kuhusu hali ya chama chao


CUF – CHAMA CHA WANANCHI
TAMKO LA WANACHAMA WA CUF MKOA WA DAR ES SALAAM JUU HALI YA KISIASA NDANI YA CHAMA.
Sisi wanachama mkoa wa Dsm,baada ya kuona hali mbaya ya kisiasa ndani ya chama na mwelekeo wa kunyongwa kwa Demokrasia ambapo maamuzi kandamizi yamejitokeza na yanatarijiwa kufanyika katika vikao vinavyoendelea hivi sasa ambavyo mazingira ya kuitishwa kwake vinaashiria dhulma zidi ya haki na utekelezaji wa matakwa ya mtu binafsi, ambapo viongozi wakuu wanaolalamikiwa hawakotayari kukosolewa badalayake wanatumia mamlaka waliyonayo kutoa maamuzi kandamizi.
Sisi kama wanachama na wapenda haki tungependa HAKI SAWA KWA WOTE ionekane ikitendeka na sio kutajwa kinadharia.
Kutokana na hali hiyo tumeona kubainisha madhaifu yaliyopo na madai yetu ya msingi tukitaraji Uziwi na Ukaidi wa Viongozi wetu utakoma hatimae Chama kuleta mvuto mpya:
A: MADAI YA MABADILIKO YA KATIBA
1. Uwepo wa Makamu mwenyekiti bara
2. Mwenyekiti Taifa na Makamu wake wawili waingie kwenye Kamati Tendaji Taifa
3. Pasiwepo ubaguzi katika uwakilishi wa wajumbe wa Wilaya wanaounda Mkutano Mkuu wa Taifa ambapo ukiondoa wajumbe wanaoingia kwa nyadhifa zao ambao Zanzibar pia uzidi, wajumbe 20 wanatoka kila Wila ya Zanzibar wakati Tanzania Bara inatoa mjumbe mmoja tu.
4. Pawepo mabadiliko katika uwakilishi wa Wajumbe wa Balaza Kuu ambapo kwa sasa ,Wajumbe 25 wanatoka Katika Wilaya 123 za Bara na Wajumbe 20 Wanatoka katika Wilaya 10 za Zanzibar.Tofauti hii ya uwiyano na ugumu wa kuhudhuria vikaoni wajumbe wanaotoka TZ Bara kutokana ubovu wa miundombinu na umbali wa maeneo wanakotoka unatoa mwanya kwa Katibu mkuu kuitisha vikao kandamizi vyenye kupitisha matakwa binafsi ya Sefu Sharif na mfumo wa upendeleo wa Wapemba
5. Mfumo wa uteuzi wa viti maalum ubadilishwe kwa kuwa unaua bara , kutokana na kuzidi kujaza wabuge Zanzibar badala TZ Bara penye hitajio kubwa la wabunge wasaidie kujenga Chama na ikizingatiwa nafasi hizo ni hesabu ya kura tulizopigania watu wa Bara kwani Zanzibar kurazao ni chache.
6. Kuendelea kwa Chama kuitumia katiba ya zamani ya toleo la 2003 wakati mkutano mkuu wa taifa wa 2010 LAND MARCK HOTEL ulipitisha katiba iliyo na vipengele vipya haitumiki mpaka hii leo ni kuvunja sheria na ushahidi wa dharau kwa wajumbe wa mkutano mkuu na wanachama matawini.
B: UTAWALA NA UTENDAJI
1. Mwenyekiti Taifa hana ofisi zanzibar wakati katibu Mkuu na makamu Mweyekiti wana ofisi Makao makuu Zanzibar na ofisi kuu bara.
2. Asilimia zaidi ya 80 ya ajira za madereva na wafanyakazi wengine wa ofisi kuu bara wanatoka zanzibar wakati hakuna madereva wanaofanya kazi zanzibar wanaotoka Bara.
3. Kuna matatizo ya mgawanyo wa raslimali za chama kati ya Bara na Zanzibar,mifano mgao wa Chama wa bajeti ya uchazi mkuu 2010 Zanzibar yenye wilaya 10 katika Mikoa 5 imepewa sh.500 milioni wakati Bara yenye wilaya 123 katika Mikoa 23 imepewa sh.70 milioni tu,fursa za Elimu na Mikopo,magali 5 ya Chama yameuzwa bila ya kufua taratibu za tenda.
C: UDHAIFU WA SEFU
1. Amekua kiongozi hodari wa kufukuza au kusababisha kuhama kwa viongozi hodari wa Tanzania Bara kama:-
(a) Mhe. James Mapalala
(b) Mhe. Maiko Nyaluba
(c) Mhe. Slivesta Kasulumbai
(d) Mhe. Geoge Shambwe
(e) Mhe. Shaibu Akwilombwe
(f) Mhe. Richard Hiza Tambwe
(g) Mhe. Wilfred Lwakatare
(h) Mhe. Othman Dunga
(i) Mhe. Asha Ngende
(j) Mhe. Khamisi Katuga
(k) Mhe. Ashura Amazi
Kwa upande wa Zanzibar ni pamoja na
a.Naila Jilawi
b.Fatuma Magimbi
c.Juma Othuman
d.Salumu Msabaha
Watu wengi waliofukuzwa au kulazimika kuhama Chama ilitokana na mfumo wenye nguvu usio rasmi ndani ya Chama unaomkinga Maalim Sefu asikosolewe
2. Toka kuanzishwa CUF hajafanya ziara au vikao hata mara moja katika mikoa na wilaya nyingi za Tanzania Bora
3. Amekuwa bingwa wa kufanya maamuzi makubwa ndani ya Chama yeye binafsi nje ya katiba na utaratibu wa vikao mfano
Kumtambua Karume na kukiuka maamuzi ya Baraza kuu la Uongozi Taifa
(a).CUF imeambulia mawaziri 7 tu CCM ina mawaziri 9 lakini wakuu wa mikoa, wakuu wilaya na watedaji wote wa serikali ni wa CCM yeye analilridhia.
(b). Ilani ya inayo tekelezwa zanzibar ni ya CCM wakati inadaiwa ni serekali ya umoja wa kitaifa
(c).Ubaguzi wa upemba ndani ya chama.
Nahaya yanayoendelea Chama kumdhibiti Mh.Hamadi Rashidi ni uthibitisho juu ya Maalim Sefu kukiburuza chama anavyotaka
a.Uundwaji wa kamati ya nidhamu na maadili kinyume na katiba ya chama.
b.kamati ya utendaji taifa imewajadili watuhumiwa bila kuwapa nafasi ya kujieleza ambapo ni haki yao kwa mujibu katiba
c.Kamati tendaji inaongozwa na Maalim Sefu akisaidiwa na wengi wa wajumbe wake ambao wameonyesha chuki za dhahiri na tayari wameshawahukumu watuhumiwa nje ya fikao mfano.E nail ya mwenye kiti wa kamati tendaji taifa sefu kwenda kwa mwenyekiti Prof.Lipumba ilishapanga namna ya kuwafukuza watuhumiwa ya 14.decembr 2012
d.Tamko la Naiba katiba mkuu bora julius mtatiro kwa press tarehe 13.12.2011 ofisi kuu buguruni la kuwatangaza watuhumiwa kuwa ni waasi na kuwapa kuwashuhulikia nje ya vikao katiba na taratibu za chama bila kuwapa nafasi ya kujieleza
e.Kauli za N.katibu mkuu Zanzibar Ismail Jusa makamu mwenyekiti Machano khamisi Ali katika maeneo mbalimbali na ofisi kuu kuwa tutawa wafukuza kama kama akina Mapalala
Hamad mwana wa haramu ni mwana wa haram tu,hata ukimuweka ndani ya chupa atatoa kidole nje ili aone kama!! Ambayo ni kashfa
c.Matumizi ya vitisho dhidi ya watuhumiwa yanadhihirisha kuwa wasioweza kutenda haki.
d.Kikao kilicho fanyika zanzibar cha kamati Tendaji ya Taifa inadhihirishwa kuwa lengo lake lilikuwa ni ubaguzi ilikikao kikifanyika yeye akawa hayupo basi kikao hicho kitaongozwa na Jusa Ismaili ambaye alisha watukana
Blue Guard Bara akiwemo mzee Juma wandwi kwamba wao ni mbwa wanatumiwa na watu wa Zanzibar katika ukumbi wa Diamond Tubilie,mwaka 2009 wakati wa mkutano mkuu
Baraza kuu limehitimishwa tarehe 4/01/2012 lina fanyika Zanzibar baada ya kikao cha kamati tendaji taifa tarehe 30 na 31 /12/2011 kutokana na mgawanyiko wa kijiografia wa wajumbe wa Baraza KuuTanzania
Baraza na hali ya miundo mbinu, Wajumbe wengi toka Tanzania Bara watashindwa kuhudhuria na hivyo kutoa nafasi ya wajumbe wa Zanzibar wanao muunga mkono sefu kufanya maamuzi kandamizi dhidi ya agenda za Tanzania bora
TAMKO LA WANACHAMA.
Sisi wanachama, tuliokutana
Leo tarehe 1. 1. 2012 tuta hamasisha wanachama miko yote na hasa Tanzania Bara kuandamana kuelekea ofisi kuu ya CUF Buguruni kupinga mipango haramu ya kufukuzwa kwa wanachama wenzetu nje ya utaratibu wa kikatiba,
Tutachukua hatua za kisheria dhidi ya viongopzi wote wanao kiuka katiba halali ya chama.
Tunatoa rai kwa baraza kuu la uongozi Taifa kulimaliza suala hili kwa njia za kusuhulishana ndani ya vikao bila kufukuzana kwa njia zilezile zilizo tumika kukaa na wauji wa CCM serekali yake waliona wanachama wa CUF Bara na visiwani katika maandamano ya januari,26 na 27 na 2001 kuliko hatua wanazo tarajia kuzichukua za kufukuzana.
…………………………………………. …………………………………….
Mwenyekiti Kamati ya Dharura Katibu Kamati ya Dharura
Hamdan Ngulangwa (0715 552699) Mpenda I. Mpenda (0715 664913)
……………………………………
Mweka Hazina kamati ya dharura
Leyla Husein (0719 827047)
Kutoka jamiiforums

SUMAYE ATAKA CCM IRUDI ZAMA ZA TANU


Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.

WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amesema CCM katika mchakato wake maarufu wa kujivua gamba, haina budi kurudia zama za TANU na kupiga vita tabia inayoota ya kununua
madaraka wakati wa uchaguzi.
Pia ameitaka Serikali iachane na nyongeza ya posho za wabunge kutoka Sh 70,000 kwa siku mpaka Sh 200,000 kwa kuwa suala hilo linaweza kumweka pabaya hata Rais.
Sumaye alisema hayo kupitia kipindi cha televisheni ya ITV cha Dakika 45 kilichorushwa juzi usiku, alipokuwa akizungumzia mambo mbalimbali ya chama na Serikali kwa Tanzania na Afrika.
Kujivua gamba “CCM iliamua kwa nia njema kuwa kuna tatizo la rushwa na ufisadi na kuwataka waliokiingiza chama katika aibu ya kutumia rushwa wajiondoe wenyewe…tafsiri yake ni
magamba yajiondoe yenyewe,” alisema Sumaye.
Alisema kama kati ya waliotakiwa kujivua magamba katika ngazi tofauti za chama hicho wako waliokataa, kazi ya chama kwa sasa ni kuwashughulikia.
“Kama kuna gamba limeng’ang’ania, basi apatikane mtu wa kulivua kwa nyuma … CCM ina watu jasiri wa kuyatoa hayo makoti (magamba), tunajua yana fedha na dhahabu lakini yakitoka hayana nguvu,” alisema Sumaye.
Alifafanua kuwa kama mtu anatumia rushwa kupata cheo, akiondolewa katika hicho cheo,
maana yake hatakuwa na pa kumfanya atumie rushwa.

“Rushwa ni balaa katika uchaguzi, hatuwezi kuchaguana kwa rushwa, lazima turudi enzi za
TANU, hakukuwa na ‘bahasha’ katika uchaguzi,” alisema na kuongeza kuwa CCM haijapambana
vizuri na rushwa.

Alifafanua kauli hiyo kuwa katika mapambano ya rushwa, kumejitokeza kambi mbili; moja ya wanaojiita wapambanaji wa rushwa wanaodaiwa kutaka kuiondoa kambi nyingine katika
ushindani.

Alihoji kwa nini hiyo kambi inayopigwa vita haisimami hata siku moja na kusema inapiga vita
rushwa na badala yake jamii inashuhudia nguvu kubwa ikijaribu kunyamazisha wanaopambana na rushwa.

“Rais Kikwete (Jakaya), aliikuta rushwa na ataiacha, tunapaswa kuendelea kupambana na
wanaonunua madaraka, mtu akiingia serikalini kwa kununua madaraka, atatafuta fedha
kununua tena kwa bei ya juu na si kuhudumia wananchi.

“Hali ni mbaya na watu wakati wa uchaguzi wamefikia hatua ya kuita wakati wa mapato, kwa
namna hii Taifa litakwisha,” alionya na kuongeza kuwa watu wamechoka na kama CCM ikishindwa iseme na wananchi wataiondoa madarakani.

Sumaye ambaye alikuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Tatu, alisema anatarajia
kazi ya kujivua gamba itafanikiwa na katika uchaguzi ujao wa ndani wa CCM utakaofanyika
mwaka huu, hakutakuwa na vitendo vya rushwa kama ambavyo imekuwa ikifanyika.

Posho na hatari kwa uongozi
Alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu nyongeza ya posho za wabunge, Sumaye alisema kwanza suala hilo halijaeleweka vizuri kwa kuwa kumejitokeza
kupingana kati ya Spika wa Bunge, Anne Makinda na Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilila, huku Ikulu ikiwa kimya.

“Kama unataka kuwa mwanasiasa mzuri, unaposimamia kitu cha maslahi yako kinachokera
wananchi, ujue umekosea,” alisema Sumaye.

Hata hivyo alionya kuwa ikiwa Serikali itabariki nyongeza hiyo ya posho, kesho yake walimu nao watataka posho na baadae watafuata wanajeshi na ikifikia huko hata Rais wa nchi hatakuwa sehemu salama.

Alikumbusha kuwa baada ya miaka mitano ya kwanza ya uongozi wa Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, wakati wa kipindi cha pili alipotakiwa kuendelea kuwa Waziri Mkuu mwaka 2000, alikataa kwa kuwa alizuia nyongeza ya posho kwa wabunge.

“Nilimwambia Rais Mkapa, usinipe hicho cheo kwa kuwa kule bungeni hawanipendi nilizuia posho zao, akaniambia nenda nikakosa la kufanya,” alisema Sumaye.

Alionya kuwa suala la posho linapukutisha mapato ya Serikali kwa kuwa hata watumishi wa
umma wameamua kuhamishia makongamano mahotelini, kila kukicha kulipana posho na kusababisha mapato yanayokusanywa na Mamlaka ya Mapato (TRA) kutoonekana yakifanya kazi.

Harakati za urais
Alipoulizwa kuhusu maneno yanayosemwa mitaani kuwa ana nia ya kugombea Urais wa
2015, Sumaye alisema hajaamua kufanya hivyo na siku akiamua, atatangaza.

“Urais lazima usubiri wakati ukifika ujipime kama unaweza na kama Watanzania wanakuhitaji
kwa nini usigombee?

“Kuwania urais si jambo baya hata ukitangaza leo, kwanza unaelezea mipango yako ya muda mrefu,” alisema na kuongeza kuwa haramu ni kutaka kumuondoa rais aliyepo madarakani au kupita pita kujaribu kufanya nchi isitawalike.

Umiliki wa mashamba Morogoro
Alipotakiwa kufafanua kuhusu mashamba anayomiliki Morogoro, kwamba anadaiwa alipora
wananchi ambao sasa hawana ardhi, alisema shamba hilo la hekta 300 halikuwa la wanakijiji.

Alifafanua kuwa shamba hilo, lilikuwa likimilikiwa na Chama cha Ushirika ambacho kililitoa
kama rehani ili kupata mkopo.

Kwa mujibu wa Sumaye, chama hicho kilishindwa kurejesha mkopo na mdai akataka
kulichukua, kikaona ili kuepuka hasara ni bora kuliuza.

“Sasa mimi kununua kitu kinachouzwa ni kosa?” Alihoji na kuongeza kuwa hata madai
kuwa ameliacha pori si ya kweli kwa kuwa kuna majani ya mifugo ambayo wanaoyaona wanadhani ni pori wakati hayatoshi kulisha mifugo yake.

CHANZO: HABARI LEO