RAIS JAKAYA KIKWETE AZINDUA JENGO LA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA FEDHA ZA SERIKALI MOROGORO


Rais Jakaya Kikwete akielekea kupanda mti baada ya kuzindua jengo jipya la Ofisi za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali la Mkoa wa Morogoro mjini Morogoro leo January 17, 2012. Pamoja naye  ni   Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali Bw Ludovick Utouh
Rais Jakaya Kikwete akizindua jengo jipya la Ofisi za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali la Mkoa wa Morogoro mjini Morogoro leo January 17, 2012. Nyuma yake ni   Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali Bw Ludovick Utouh na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Joel Bendera
Rais Jakaya Kikwete akikata utepe kuzindua jengo jipya la Ofisi za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali la Mkoa wa Morogoro mjini Morogoro leo January 17, 2012. Kushoto  yake ni   Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali Bw Ludovick Utouh na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Joel Bendera …
Rais Jakaya Kikwete akipokea zawadi  toka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali Bw Ludovick Utouh katika hafla ya uzinduzi wa  jengo jipya la Ofisi za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali la Mkoa wa Morogoro mjini Morogoro leo January 17, 2012. wengine ni Waziri wa Katiba Mh Celina Kombani (wa pili kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Joel Bendera na mkuu wa Wilaya ya Morogoro.
Picha na IKULU

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL MGENI RASMI SHEREHE ZA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA WA KICHINA DAR ES SALAAM


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina, zilizoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara wa Kichina nchini (CBCT), zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana jioni Januari 15

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea mfano wa Hundi, yenye thamani ya Sh. Milioni 16, kutoka kwa Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng, (kulia) iliyotolewa na City Bank Tanzania LTD kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyotokea jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana, ikiwa  ni sehemu ya sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam jana Januari 15.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea mfano wa Hundi, yenye thamani ya Sh. Milioni 10, kutoka kwa Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng, (kulia) iliyotolewa na Chama cha Wafanyabiashara wa Kichina wa Tanzania (CBCT) kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyotokea jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana, ikiwa  ni sehemu ya sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam jana Januari 15. Picha na Muhidin Sufiani-OMR