Waliofutiwa Matokeo Kurudia Baada Ya Miaka Mitatu


Na Fatma A Mzee Habari Maelezo 15/2/2012

 

Katibu mtendaji wa baraza la Taifa la mitihani Tanzania (NECTA), Dkt Joyce L. Ndalichako ameeleza kuwa jumla ya wanafuzi 3303 wamefutiwa mitihani yao kutokana na kuthibitika kufanya udanganyifu.
DK. Joyce liyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Bwawani mjini zanzibar.
Aliongeza kuwa kati ya hao kuna baadhi ya watahiniwa wameandika matusi katika karatasi zao kamitihani na wengine kuwacha maswali na kutokujibu kabisa maswali ya majibu hayo. Hata hivyo Dkt Joyce alishindwa kujibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari kutokana na kutokufanya majumuisho yote ya mitihani hiyo iliyofanyika nchini.Aidha alieleza kuwa suwala hilo la udanganyifu linafanyika katika makundi yote matatu ambao ni walimu wazazi pamoja na wanafunzi wenyewe.
Dkt Jooyce ameongeza kuwa waliofutiwa mitihani kulitokana na kikao cha 86 nambari 6 B kilichofanyika tarehe 7-2-2012. Kanuni za baraza la mitihani zinazoeleza kuwa watahiniwa hao hawataruhusiwa kufanya mitihani kwa muda wa miaka mitatu.
Hata hivyo amesema kuwa baraza limewaonea huruma kwa kuwapa hukumu hiyo kwani katika kanuni za NECTA wanafunzi wanaofutiwa mitihani hawaruhusiwi kufanya mitihani tena.
Pia katibu mtendaji huyo aliwataka wasimamizi kuwa makini katika kazi zao na kusimamia kwa uwangali mitihani kwani udanganyifu huwa unamadhara makubwa katika taifa ambapo kutazalishwa wataalamu wasio na viwango hasa katika kipindi hiki ambapo tunaingia katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Wakati huo huo chuo kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kimewasimamisha wanafunzi watatu wa chuo hicho baada ya kubainika walitumia vyeti vya kughushi wakati walipojiunga na chuo hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari katika chuo hicho, Vuga mjini Zanzibar, mwanasheria wa SUZA Mtaibu Abdalla Othman amewataja wanafunzi hao kuwa ni Mahfoudhat Hassan Khamis anaesoma digrii ya sanaa, Shafii Suleiman Mringo anaesoma cheti cha teknolojia ya habari na Yussuf Khamis anaesoma cheti cha sayansi ya komputa.

NBC YANUNUA HISA ASILIMIA 10.87 KWENYE KAMPUNI YA MIKOPO YA NYUMBA, TMRC


Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya NBC Bw. Lawrence (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi bilioni moja kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Mortgage Refinance Company Limited (TMRC) Bw Rished Bade katika hafla iliyofanyika kwenye makao makuu ya benki hiyo leo.Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) leo imekabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi bilioni moja kwa Kampuni mahususi ya Kutafuta Fedha na Kutoa Mikopo ya Muda Mrefu ya Nyumba iitwayo Tanzania Mortgage Refinance Corporation (TMRC) ikiwa ni kiasi cha kununua hisa za asilimia 10.87 kwenye kampuni hiyo. TMRC ni taasisi ya kifedha inayomilikiwa na mabenki mbali mbali kwa lengo la kusaidia mabenki yaweze kutoa mikopo ya muda mrefu ya nyumba kwa wateja. Lengo kuu la TMRC ni kusaidia kutoa fedha kwenye soko la kifedha la Tanzania kwa ufanisi, na kuzilenga fedha hizo kwa mabenki wanachama kwa viwango vya ushindani. Hii itawezesha upatikanaji wa makazi kwa watanzania, na pia kuchangia maendeleo ya masoko ya mitaji. Shughuli hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki ya NBC, ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bwana Lawrence Mafuru. Akizungumza kwenye tukio hilo, Bwana Mafuru alisema: “Tunaamini kuwa fedha hizi zitaiaidia TMRC katika juhudi zake za kuwawezesha Watanzania wapate kumiliki makazi bora. Kitendo hiki kinaonyesha dhamira ya NBC katika kusaidia sekta ya mikopo ya nyumba Tanzania ” Hundi hiyo imepokewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TMRC, Bwana Rished Bade mbele ya viongozi wa ngazi ya juu wa kampuni hiyo pamoja na wawakilishi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Mwezi Oktoba 2011, NBC pamoja na benki nyingine sita zilisaini mkataba na Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) kwa ajili ya kuwawezesha Watanzania kipata makazi bora zaidi