TAMKO LA BUNGE KUHUSU POSHO KUHUSU POSHO ZA WABUNGE


Dr. Thomas D. Kashililah-Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA TAARIFA KWA UMMA
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa iliyotolewa na baadhi ya Vyombo vyaHabari na baadhi ya Wabunge kuwa posho ya Vikao vya Bunge imeongezekakutoka Sh.70,000/= hadi 200,000/=.
Suala la mabadiliko ya Posho ya Vikao vya Bunge lilijitokeza katikaMkutano wa Wabunge, tarehe 8 Novemba, 2011 walipoiomba Serikali iangalie upya suala hili kwa lengo la kuboresha. Hadi tunapotoa tangazo hili,
Serikali haijatoa taarifa iwapo Posho hiyo imeongezeka kutoka Sh.70,000/=hadi 200,000/=Tunasikitika na kushangaa sana kwa kauli hii kwani ina lengo la
kujenga chuki baina ya Wabunge na Wananchi wao waliowapigia kura.

Kwa mujibu wa Waraka wa Rais kuhusu Masharti ya Mbunge uliotolewa tarehe 25 Oktoba, 2010 wenye Kumb. Na. CAB111/338/01/83 na kusainiwa na Katibu

Mkuu Kiongozi, pamoja na stahili zingine, Mbunge anastahili kulipwa Posho

ya Kikao ambayo ni sawa na Sh.70, 000/= kwa kila kikao na masharti hayo

hayajafanyiwa marekebisho wala kufutwa.
Kwa hiyo, taarifa hiyo iliyotolewa siyo sahihi na imelenga kuleta chuki baina ya Wabunge na Wananchi. Endapo itatokea mwenye mamlaka kupitisha kiwango kipya cha Posho ya Vikao vya Bunge, itakuwa ni uamuzi kama uamuzi mwingine anaoutoa wa kuwaongezea Watumishi wa umma mishahara, posho, marupurupu na mafao mengine.
Ofisi ya Bunge inahidi kufanya kazi kwa ushirikiano na Vyombo vya Habari kwa lengo la kuleta ufanisi mzuri na kujenga mahusiano mazuri ya kuaminiana kati ya Wabunge, Vyombo vya Habari na Wananchi.
Imetolewa na: Dr. Thomas D. Kashililah
KATIBU WA BUNGE

Vodacom Tanzania Yazindua Kampeni Ya Share and Care


MICHEZO.

Meneja wa kitengo cha m pesa kanda ya pwani wa Vodacom Tanzania Nabwike Kibona akimtayarishia chai Ramadhani Abdalah ambae ni mtoto yatima wa kituo cha Mwana Orphans Centre cha Vingunguti wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Share and Care ambayo huwa inafanyika kila mwisho wa mwaka kwa ajili ya kuwasaidia mahitaji mbalimbali watoto yatima kuelekea msimu wa sikukuu ya krismas,Vodacom imetoa jumla ya msaada wa thamani ya shilingi hamsini katika kampeni hiyo.
Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Mary Natema akiwanywesha juisi baadhi ya watoto yatima waliohudhulia uzinduzi wa kampeni ya Share and Care ambayo huwa inafanyika kila mwisho wa mwaka kwa ajili ya kuwasaidia mahitaji mbalimbali watoto yatima kuelekea msimu wa sikukuu ya krismas,Vodacom imetoa jumla ya msaada wa thamani ya shilingi Milioni hamsini katika kampeni hiyo.
Meneja wa kitengo cha m pesa kanda ya pwani wa Vodacom Tanzania Nabwike Kibona akiwahudumia watoto yatima wa kituo cha Mwana Orphans Centre cha Vingunguti wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Share and Care ambayo huwa inafanyika kila mwisho wa mwaka kwa ajili ya kuwasaidia mahitaji mbalimbali watoto yatima kuelekea msimu wa sikukuu ya krismas,Vodacom imetoa jumla ya msaada wa thamani ya shilingi Milioni hamsini katika kampeni hiyo.
Ofisa Mkuu wa Masoko na Uhusioano wa Vodacom Tanzania akiongea jambo na Mkurugenzi rasilimali watu wa Vodacom Stela Chiwango pamoja na Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Share and Care ambayo huwa inafanyika kila mwisho wa mwaka kwa ajili ya kuwasaidia mahitaji mbalimbali watoto yatima kuelekea msimu wa sikukuu ya krismas,Vodacom imetoa jumla ya msaada wa thamani ya shilingi Milioni hamsini katika kampeni hiyo.
Mkuu wa kitengo cha kusaidia jamii cha Vodacom Tanzania”Vodacom Foundation”Yessaya Mwakifulefule akitwishwa kiroba cha Maharage na Meneja Uhusiano na Habari za Mtandao wa kampuni hiyo Matina Nkurlu kushoto na Meneja wa akaunti na usajili wa namba za simu Loius Maro,wakati wa kupakua mizigo hiyo tayari kwa kuwagawia msaada vituo mbalimbali vya watoto yatima jijini Dares salaam kwenye uzinduzi wa kampeni ya Share and Care ambayo huwa inafanyika kila mwisho wa mwaka kwa ajili ya kuwasaidia mahitaji mbalimbali watoto yatima kuelekea msimu wa sikukuu ya krismas,Vodacom imetoa jumla ya msaada wa thamani ya shilingi Milioni hamsini katika kampeni hiyo.
Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania kitengo cha magari George Madinda, akipakia baadhi ya misaada mbalimbali kwenye gari tayari kwa kupeleka kwenye vituo mbalimbali vya watoto yatima vya jijini Dares Salaam hapo jana wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Share and Care ambayo huwa inafanyika kila mwisho wa mwaka kwa ajili ya kuwasaidia mahitaji mbalimbali watoto yatima kuelekea msimu wa sikukuu ya krismas,Vodacom imetoa jumla ya msaada wa thamani ya shilingi Milioni hamsini katika kampeni hiyo.
Watoto yatima wa kituo cha Friends of Don Bosco kilichopo kimara wakibeba msaada wa vitu mbalimbali vilivyotolewa na wafanyakazi wea Vodacom Tanzania wakati wa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Share and Care ambayo huwa inafanyika kila mwisho wa mwaka kwa ajili ya kuwasaidia mahitaji mbalimbali watoto yatima kuelekea msimu wa sikukuu ya krismas,Vodacom imetoa jumla ya msaada wa thamani ya shilingi Milioni hamsini katika kampeni hiyo,wanaoshuhudia ni wafanyakazi wa kampuni hiyo kitengo cha huduma kwa wateja.
Mtoto yatima wa kituo cha T.H.M.H cha Magomeni jijini Dare Salaam Rebeca Elias akiwa ameshikilia mbuzi mara baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi rasilimali watu wa Vodacom Tanzania Stela Chiwango aliemshika begani na Ofisa Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa kampuni hiyo Mwamvita Makamba watatu toka kulia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Share and Care ambayo huwa inafanyika kila mwisho wa mwaka kwa ajili ya kuwasaidia mahitaji mbalimbali watoto yatima kuelekea msimu wa sikukuu ya krismas,Vodacom imetoa jumla ya msaada wa thamani ya shilingi Milioni hamsini katika kampeni hiyo,wanaoshuhudia ni wafanyakazi wa kampuni hiyo kitengo cha huduma kwa wateja.
Mkurugenzi rasilimali watu wa Vodacom Tanzania Stela Chiwango akimkabidhi mbuzi mmoja wa watoto yatima wa kituo cha Friends of Don Bosco kilichopo kimara jijini Dares Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Share and Care ambayo huwa inafanyika kila mwisho wa mwaka kwa ajili ya kuwasaidia mahitaji mbalimbali watoto yatima kuelekea msimu wa sikukuu ya krismas,Vodacom imetoa jumla ya msaada wa thamani ya shilingi Milioni hamsini katika kampeni hiyo,wanaoshuhudia ni wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja tayari kuelekea katika vituo mbalimbali vya watoto yatima vya jijini Dares Salaam mara baada ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya Share and Care hapo jana ambayo huwa inafanyika kila mwisho wa mwaka kwa ajili ya kuwasaidia mahitaji mbalimbali watoto yatima kuelekea msimu wa sikukuu ya krismas,Vodacom imetoa jumla ya msaada wa thamani ya shilingi Milioni hamsini katika kampeni hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwahudumia chakula baadhi ya watoto yatima wa vituo mbalimbalivya jijini Dares Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Share and Care ambayo huwa inafanyika kila mwisho wa mwaka kwa ajili ya kuwasaidia mahitaji mbalimbali watoto yatima kuelekea msimu wa sikukuu ya krismas,Vodacom imetoa jumla ya msaada wa thamani ya shilingi Milioni hamsini katika kampeni hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakicheza pamoja na watoto yatima wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Share and Care hapo jana ambayo huwa inafanyika kila mwisho wa mwaka kwa ajili ya kuwasaidia mahitaji mbalimbali watoto yatima kuelekea msimu wa sikukuu ya krismas,Vodacom imetoa jumla ya msaada wa thamani ya shilingi Milioni hamsini katika kampeni hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja tayari kuelekea katika vituo mbalimbali vya watoto yatima vya jijini Dares Salaam mara baada ya uzinduzi rasmi wa kampeni ya Share and Care hapo jana ambayo huwa inafanyika kila mwisho wa mwaka kwa ajili ya kuwasaidia mahitaji mbalimbali watoto yatima kuelekea msimu wa sikukuu ya krismas,Vodacom imetoa jumla ya msaada wa thamani ya shilingi Milioni hamsini katika kampeni hiyo.

Benki ya Twiga Kutumia Miundombinu ya Benki Ya Posta Kutoa Huduma za Kifedha


C E O wa Twiga Bank, Hussein Mbululo akiongea na waandishi wa Habari

KATIKA jitihada za kuboresha huduma za kibenki na kusogeza huduma zaidi kwa wateja, Benki ya Twiga Bancorp Limited inaanzisha ushirikiano na Benki ya Posta Tanzania kutoa huduma ya kusafirisha pesa (monygram).
Akiongea  katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (sabasaba) ambako benki ya Twiga inashiriki maonesho ya miaka 50 ya uhuru, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Twiga, Hussein Mbululo alisema katika juhudi za benki ya Twiga kuboresha huduma na kuzifanya kuwa za uhakika, benki hiyo imeamua kwa kanzia kutumia miundombinu ya benki ya Posta Tanzania kuwafikia wateja wake.
Amesema utaratibu huo utaanza kutumika mapema mwaka ujao.
“Kufuatia kuongezeka kwa ushindani katika biashara ya kutuma pesa, benki yetu imeamua kujizatiti kwa kutumia mtandao wa benki ya posta kufikisha huduma kwa wateja wote kote nchini, hii itasaidia kufanya huduma zetu kuwa nzuri na za uhakika,” alisema Mbululo.
Alisema utaratibu wa kutuma pesa kwa njia ya moneygram ni huduma ya pekee inayotolewa na benki ya Twiga na kwamba unamuwezesha mteja kutuma na kupokea pesa akiwa nje na ndani ya nchi.
Benki ya Twiga pia inatoa huduma za fedha kwa kutumia mtndao wa Umoja Switch Automatated Teller Machine.
Kwa mujibu wa Mbululo, benki ya Twiga ilianzishwa mwaka 1992, wakati huo ikiitwa National Bureau De Change.
Hata hivyo mwaka 1998, beni ya Twiga ilibadilishwa na kuwa benki isiyopokea amana lakini ikajikita zaidi katika kutoa huduma za kibenki.
Akielezea mafanikio ya benki hiyo, Mbululo alisema Twiga imekuwa benki pekee ya wazawa ambayo imeweza kustahimili changamoto mbalimbali katika ushindani pasipo kutegemea ruzuku kutoka serikalini.
Alisema mbali na kutengeneza faida kubwa kila mwaka, kufikia Sepemba, 2011 benki ilikuwa imepokea kiasi cha Sh 50 billioni kutoka kwa wateja na kutoa mikopo ya kiasi cha Sh 30 billioni.
Mbululo aaliongeza kuwa, benki ya Twiga ambayo kwa sasa ina matawi manne, Dar es Salaam, Mwanza na Arusha inafanya mandalizi ya kufungua matawi zaidi katika mkoa wa Dodoma na Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Aidha, Mbululo alihaidi kuwa benki yake itaendelea kusimamia na kuwasaidia wajasiriamali wadogowadogo (SMEs) kwa kuwapatia mikopo yenye masharti nafuu naya uhakika kwani ndio hasa kichocheo cha ukuaji wa uchumi nchini.
Kwamujibu wa Mbululo benki inajipanga kuzidi kujiimarisha kwa kuboresha huduma mbalimbali ili kuendana na wakati na kuhimili ushindani kutoka kwa benki zaidi 40 za kibiashara hapa nchini.
Ameongeza kuwa, benki inawashauri na kuwataka wananchi kufungua na kutumia akaunti za watoto yaani ‘Twiga Kids Account na ile ya Holiday Account’ ambazo zimeanzishwa hivi karibuni kwa madhumuni ya kuwasaidia wazazi na walezi kuwawekea akiba watoto wao pamoja na kuweka fedha kwaajili ya safari za mapumzikoni na wakati huu wa siku kuu.

Utakuwa Wapi December Tisa Mtanzania wa DC ?


Tarehe 9, December ni sherehe za uhuru wa Tanganyika ambao wengi wetu tumebadilisha na kuita uhuru wa Tanzania. Ni uhuru upi ni swala ambalo tutalijadili siku nyingine. Leo ningependa kuomba tujiangalie sisi watanzania wa Washington Metropolitan, je tutakuwa wapi December 9, 2011?.
Kwa uhakika kabisa inaonekana watanzania wa baadhi ya states kadhaa hapa USA kama New York, Delaware, Illinois, nk na nchi nyingi wamejipanga na wengi wao wamejiweka pamoja kama jumuia au kushirikiana na balozi zao kuadhimisha sherehe za uhuru siku ya tarehe 9, December.
Nina uhakika kabisa siku hiyo ya Ijuma wengi wetu tutakuwa makazini tukiwajibika na baadaya hapo tutarejea majumbani bila hata kukumbuka kwamba ni siku ambayo tuliachiwa uhuru wetu wa Waengereza.
Ukiangalia kiundani na kutafakari si kwamba ati sisi si wazalendo wa nchi yetu, na sio kwamba hatutaki kusherherekea sherehe hizi, au kujumuika pamoja bali tumekumbwa na mawimbi ambayo yanatutatiza na yanatufanya tushindwe kuliongoza jahazi letu wenyewe.
Kama Tutakumbuka ni kwamba tarehe 23, September kuliadhimishwa sherehe za uhuru hapa wahington DC, kupitia Ubalozi wetu hapa na Diaspora Council of Tanzanians in America (DICOTA), ambao wengi wetu tulilalama na kuweweseka kwanini sherehe za uhuru zinafanyika September na kwa nini tulipie kwenda kwenye sherehe za uhuru wetu.
Malalamiko yetu yalikuwa ya haki kabisa na yakimsingi lakini kwa vile tulikuwa tukisema mmoja mmoja na huku tukiwa nje, tulishindwa kuyafikisha yanako husika, na hatima yake sisi kama wakazi wa hapa tulionekana kuwa tulikuwa wababaifu na tuna puza mazungumzo.(Baseless).
Sasa kongamano la DICOTA lishapita na watu wote pamoja na wageni wa heshima wamerudi makwao na wanajianda kushereherekea sherehe za uhuru haswaa tarehe 9, December. Sie wa DC tupo na tumebaki tunauliza nini kimetokea na inakuwaje tumebaki kwenye hali hii.
Nakubaliana na mawazo ya wengine wanaosema kwamba maisha si yanaendelea kwani tatizo nini ?. Swali langu ni kwamba je sisi kama wana DC tutakuabli watu wafanye maamuzi kwa ajili yetu? Wafanye mambo ambayo yanaonekana yamefanywa hapa DC wakati sisi wakazi wa hapa hatukuhusihswa, husika au kukaribia. Wakitengemeza ni kheri , je wakiboronga ? . Tukae tukijuwa kwamba hatuwei kuishi kama mchanga “ Kadri unavyo ubana mkononi ndio unazidi kupungua kupitia vidoleni”.
Martin Luther King Says, “Take the First Step. You Don’t Have to See the Whole Staircase, Just Take the First Step”.
Wenu Wa DC Iddi Sandaly