Rais Jakaya Anunua Shati La Batiki…


Hapa sasa anatoa pesa...

Hapa Mheshimiwa Rais kikwete anajipima kwa aina yake...

Rais Jakaya Kikwete,akipimwa shati la batiki na mpambe wake, huku naye akijipima na hatimaye kulinunua kwa kulipa sh.30,000 kwa Mjasiriamali Tasiano Tungaraza jana katika maonesho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam. Tungaraza ni miongoni mwa Wajasiriamali waliokuwa banda la Ofisi ya Ikulu ambao wamewezeshwa na Mpango wa Kurasimisha Rasirimali za Wanyonge na Biashara MKURABITA).Picha na Mdau Richard Mwaikenda.

NAPE NNAUYE AKABIDHI MATREKTA KWA WAKULIMA


Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akijaribu kuliendesha trekta kabla ya kukabidhi matrekta mawili kwa wakulima wa Kata ya Kwadelo, wilaya ya Kondoa mkoani Singida, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Dar es Salaam, leo...

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akimkabidhi matrekta mawili diwani wa Kata ya Kwadelo mkoani Singida, Omari Kariate, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo. Trekta hizo ambazo ni mkopo kutoka Shirika la SUMA JKT, ni kwa ajili ya wakulima wa Kata hiyo. Wengine pichani ni Wajumbe kutoka Chama Cha Wakulima wa Kata hiyo waliohudhuria makabidhuano hayo. (Picha na Bashir Nkoromo).

NA MWANDISHI WETU

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Itikadi na Uenezi Nape Nnauye amewataka viongozi kuongoza kwa vitendo badala ya maneno.

Nape alisema hayo wakati akikaidhi matrekta mawili kwa wakulima wa Kata ya Kwadeo wilaya ya Kondoa mkoni Singida, katika hafla iliyofanyika leo Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba mjini Dar es Salaam.

Wakulima wamepata matrekta hayo kwa mkopo kutoka Shirika la Suma JKT, kupitia mpango wa kuhamasisha kilimo cha kisasa unaosimamiwa na diwani wa kata yao ya Kwadelo, Omari Kariate.

Wamefanikiwa kukokpeshwa matrekta baada ya kuweza kulipa asilimia 50 ya gharama yote ya ununuzi ambayo trekta moja ni sh. milioni 25.

“Ili mapinduzi ya kweli yaweze kufikiwa katika kilimo na sekta nyingine za maendeleo ni lazima sasa viongozi waepuke mtindo wa kufanya kazi wa nadahria tu, badala yake wajikite katika kuonyesha vitendo, diwani huyu ameonyesha mfano mzuri wa kuingwa”, alisema Nape.

Nape alisema hatua ya diwani huyo kuanzisha mpango na kuuhamasisha kwa wananchi hadi kukubalika na kuweza kutoa matunda si jambo la mzaha ni suala la dhamira ya kweli katika uongozi.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, diwani wa Kata hiyo, Kariate alisema, mpango wake wa kuhamasiaha wakulima kuwezeshwa kutumia matrekta umeanza kuonyesha mafanikio kwa kuwa sasa kata hiyo ina jumla ya trekta tisa zote za mkopo kutoka SUMA JKT.

Alisema, kupitia mpango huo sasa wakulima wa kata hiyo wanaweza kulima kisasa zaidi na hivyo kujipatia mavuno mengi kuliko kutumia jembe la mkono. wilaya ya Kondoa hulima mazao ya mahindi, uwele na alizeti

Pre – New Year Eve Party Usiku wa Bongo Flava na Dj Dave Fresh From Tz Kny, Ugan, Rwnd and Burnd Tour.


    The Swahilli Entertainments well comes you Pre New year eve party Dec 30th

    Usiku wa bongo flava na Dj Dave fresh from Tz Kny, Ugan, Rwnd and Burnd tour.
    Along with Dj Luke & Dj Seif, well come back on the stage D.H The entertainer performer his new hits. remembrance of Bongo flava Super Star Mr Ebo R.I.P you will always be with us and this night we will pay our respect and perform his signature tunes by D.H The entertainer .

    Same night we will premier number one hit Bongo Flava in Tanzania ( hakunaga by Suma Lee) Let super star shine DH The entertainer will perform this tune.
    Please come early door open 10p bar close @2:30A. Door $10, ladies $5 B4 11P. Drinks special all night long.
    4400 Rhode Island Ave Brentwood, MD 20722