MAMBO MATATA KUTOKA KWAFLAVIAN MATATA …


 On behalf of the Flaviana Matata Foundation and Tanzania Mitindo, we would like to take this opportunity to thank Russell Simmons for his kind donation of auction items and cash for our annual charity event, Tanzania Red Ribbon Fashion Gala 2011 which took place on World Aids Day, December 11.The items he donated raised 7,700,000 tanzanian shillings and this year the event raised 56,000,000 tanzanian shillings in its entirety.

 The fund will be used to establish Tanzania Mitindo House training centre for teenage orphans that will train and empower them economically.


The centre aims to train at least 100 teenage orphans from different orphanages in Dar es salaam each year. The centre will offer courses on life skills, education, fashion designing, tailoring, arts and crafts, hair and make up, computer skills and graphic designing.We believe one can pay back the loan of GOLD but one dies forever in DEBT to those who are KIND to them.

We at Flaviana Matata Foundation and Tanzania Mitindo House appreciate your contribution in succeeding the goal of helping and creating a better life for Tanzanian children.Thank you very much.

Swahili Center yamtunikia Dr. Karume nishani ya ‘Shujaa wa Zanzibar’‏


Swahili Center yamtunikia Dr. Karume nishani ya ‘Shujaa wa Zanzibar’‏

Kituo cha Sanaa za Maonesho za Waswahili (Swahili Performing Arts Center) Zanzibar kimemtunukia Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mhe. Dr. Amani Karume, nishani ya ‘Shujaa wa Zanzibar’ ikiwa ni hatua ya mwisho katika kuadhimisha kufikiwa kwa maridhiano na hatimaye serikali ya umoja wa kitaifa nchini Zanzibar.

Dr. Karume alikabidhiwa nishani hiyo na mwanasiasa mkongwe Mzee Hassan Nassor Moyo siku ya Ijumaa tarehe 23 Desemba 2011 katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwake huko Mbweni nje kidogo ya Mji Mkongwe.

Akiwasilisha risala yake katika tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Swahili Performing Arts Center Kheri Jumbe alitoa shukrani kwa Dr. Karume kutokana na jitihada zake katika kuleta amani ya kudumu nchini Zanzibar.

Jumbe alieleza kuwa, taasisi yake iliona umuhimu wa kuandaa sherehe za maridhiano kupitia mradi wa sanaa uliopewa utambulisho wa 100% Zanzibari (Mzanzibari asilimia moja) ili kuwaenzi waasisi wa maridhiano hayo na kueliimisha wananchi juu ya umuhimu wake.

“Kwa kipindi cha miezi miwili kuanzia Oktoba 4 hadi Desemba 3, tumekwenda katika mikoa yote ya Zanzibar na kuwasilisha ujumbe juu ya umuhimu wa kuimarisha misingi ya umoja na kuweka mbele uzalendo, ‘ alisema Jumbe.

Akikabidhi nishani hiyo kwa Rais mstaafu, Mzee Hassan Nassor Moyo alirejea wasia wake wakutaka viongozi wakuu wa Zanzibar kutowavumulia watendaji wa serikali wanaovuruga maridhiano.

Katika kuipokea nishani hiyo, Dr. Karume aliwapongeza watendaji wa Swahili Center pamoja na wasanii walioshirki katika mradi huo kwa juhudi zao katika kuyaendeleza maridhiano kupitia sanaa zilizobeba ujumbe huo.

Nishani kama hiyo ya ‘shujaa wa Zanzibar’ alitunukiwa pia Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad katika kilele cha sherehe za maridhiano huko uwanja wa Gombani, kisiwani Pemba tarehe 3 Desemba 2011.

Waliohudhuria katika uwasilishwaji wa nishani hiyo kwa Dr. Karume ni Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe, Mhe Ismail Jussa pamoja na Mkurugenzi wa Sanaa was Swahili Center, Mahsin Basalama.

Kupitia mradi wa 100% Zanzibari wasanii 130 kutoka vikundi 11 vya sanaa za maonesho walishiriki katika kambi za kjenga umoja na kufanya maonesho nchini kote. Mradi wa 100% Zanzibari umedhaminiwa na Ubalozi wa Norway pamoja na kampuni ya mawasiliano ya Zantel.

Kituo cha Sanaa za Maonesho za Waswahili (Swahili Performing Arts Center) Zanzibar kimemtunukia Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mhe. Dr. Amani Karume, nishani ya ‘Shujaa wa Zanzibar’ ikiwa ni hatua ya mwisho katika kuadhimisha kufikiwa kwa maridhiano na hatimaye serikali ya umoja wa kitaifa nchini Zanzibar

.

Shivji amkosoa JK kuhusu katiba…


MWENYEKITI wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere Profesa Issa Shivji amekosoa Sheria ya Mchakato wa Kuundwa kwa Katiba mpya iliyosainiwa na Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni na kusema kuwa ni mbovu na haitazaa katiba bora.
Novemba 29 mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete alitia saini Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 huku kukiwa na malumbano makali kutoka asasi za kiraia, vikiwemo vyama vya siasa, kupinga hatua hiyo kwa maelezo kwamba, mchakato huo uliendeshwa kwa mizengwe na Hata hivyo, taarifa ya kusainiwa muswada huo iliyotolewa na Ikulu kwa vyombo vya habari, ilieleza kuwa hatua hiyo ya Rais Kikwete, ilikamilisha safari ya kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 baada ya Bunge kupitisha muswada huo uliowasilishwa na Serikali huku ikiweka wazi kuwa Serikali itaendelea kusikiliza maoni na mawazo ya wadau na wananchi mbalimbali kuhusu namna ya kuboresha sheria hiyo.
‘’ Mheshimiwa Rais Kikwete anatoa wito kwa mwananchi yeyote mwenye maoni ama mawazo ya namna ya kuboresha Sheria hiyo, ajisikie yuko huru kutoa maoni yake na Serikali itasilikiza na kuchukua hatua zipasazo’’ ilieleza sehemu ya taarifa hiyo iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu Akizungumza katika kipindi cha Kipima Joto kinachorushwa na kituo cha televisheni ya ITV juzi usiku, Profesa Shivji ambaye ni mmoja wa magwiji wa sheria hapa nchini, alisisitiza kuwa sheria hiyo ni mbovu na kamwe haitazaa katiba bora wanayoitaka wananchi na kuwashauri kwenda kupinga jambo hilo mahakamani.

Akichambua sheria hiyo, Profesa Shivji alikosoa kifungu cha 21 akisema kuwa inashangaza kwani kinazuia hata watu kuikosoa sheria hiyo. “Mimi nasema kuwa sheria hii ni mbovu…Katika sheria hii, kifungu hiki kinanizuia hata kusema, sheria hii ni mbovu’. Mimi sijui kulikuwa na fikra gani kuweka kifungu kama hiki, kitu kimoja tu ni kwenda mahakamani kuipinga.
” Alisema. 

Akichambua kifungu kimoja baada ya kingine katika sheria hiyo, Profesa Shivji alisema kuwa imewatenga kabisa wananchi katika mchakato mzima wa kuandikwa kwa katiba mpya.
“Wananchi wanatakiwa kushirikishwa tangu hatua ya kwanza, kwa mchakato wa Bunge, yaani sisi wenyewe tumeshirikishwa kupitisha sheria hiyo kuhakikisha vyombo vyote vinavyohusika vinafuatwa.” Alisema Profesa Shivji.

Akitoa mfano wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya Katiba, Profesa Shivji alisema kuwa, haikufanya kazi yake kikamilifu hivyo kuwanyima wananchi fursa ya kutoa maoni. “Tulianza awali lakini hatukukamilisha…hatukuwa na sababu ya kutokukamilisha.
Tulipoanza kwenye makongamano yale yaliyofanyika tulipata maoni ya wananchi, baada ya kupata maoni, ndipo mchakato wa kuunda katiba,’’ alisema Tume ya Rais ya Katiba Kuhusu Tume ya Rais ya Kuunda Katiba, Profesa Shivji, alisema haipaswi kuwa moja kwa moja chini ya Rais bali pia ishirikishe wananchi. 


Alitoa mfano wa tume ya aliyewahi kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Edwin Mtei iliyoshughulikia Marekebisho ya Fedha na Tume ya Rais ya Ardhi lakini akasema, Tume ya Katiba siyo ya rais, Hii siyo Tume ya Rais, ni Tume ya Katiba (Constitutional Commission), inayoundwa chini ya sheria zilizopitishwa na Bunge. Hata tume iliyounda Katiba ya mwaka 1977 iliundwa chini ya Mkataba wa Muungano.
Sheria ile ilitaja wazi kwamba rais akikubaliana na Rais wa Zanzibar, ataunda Tume ya Katiba” alisema. Aliendelea kusisitiza ushirikishwaji wa wananchi katika tume hiyo akisema kuwa rais anapaswa kuzingatia maoni ya wananchi katika uteuzi wa wajumbe wake.
“Mfano taasisi mbalimbali za jamii zetu, taasisi za serikali, vyombo vya habari, vyuo vikuu, wanaweza kupendekeza majina mawili, tunaona kwamba hawa watu wanafaa kuwa wajumbe, halafu rais anateua kupitia hayo. 

Hiyo ndiyo namna ya kuwashirikisha wananchi lakini kwa sheria ya sasa hatujui rais anatumia vigezo gani,” alisema.
Bunge la Katiba Kuhusu Bunge la Katiba, alisema idadi ya wajumbe 600 wa Bunge hilo ni kubwa mno ukilinganisha na idadi ya Watanzania 40 milioni, hali ambayo alisema italifanya Bunge hilo kutumia gharama kubwa bila sababu. Alitoa mfano wa Bunge lililounda katiba ya uhuru ya India la mwaka 1947 akisema lilikuwa na wajumbe 250 na wakati huo idadi ya wananchi wakiwa 100 milioni.
Alikosoa pia uwiano wa idadi ya wajumbe hao akisema kuwa kati yao, teluthi mbili, yaani wajumbe 400 watakuwa ni wa CCM. Akasema hali hiyo itawanyima fursa wananchi ambao si wanachama wa vyama vya siasa. Kura ya maoni Kwa mujibu wa Profesa Issa Shivji, japo wananchi watapata nafasi ya kupiga kura ya maoni, bado kuna hatari ya kutopata katiba bora kwani hawakupata nafasi ya kutosha ya kutoa maoni yao. 


“Katiba inaweza kuwa na ibara 500, inawezekana kati ya hizo hupendi ibara mbili tu. sasa ukisema hapana ndiyo umeikataa katiba yote kwasababu hatukufuata vizuri mchakato,” alisema na kuongeza; “Hata Hitler aliingia madarakani kwa kura ya maoni”.
Aliongeza kuwa kuna hatari katiba ikapitishwa na idadi ndogo ya wananchi hasa kutokana na tabia ya wananchi kutopenda kupiga kura.
“Sheria hiyo inasema kuwa asilimia 50 ya waliopiga kura siyo waliojiandikisha. Unaweza kukuta katiba ikapitishwa na asilimia 20 tu ya wananchi”.


Mjadala huo pia uliwahusisha Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama cha UDP, Isaac Cheyo ambao pia waliipinga sheria hiyo. Kwa upande wake Mnyika alieleza sababu ya wabunge wa Chadema kususia mjadala wa katiba na kutoka nje ya ukumbi wa Bunge akisema kuwa walipinga muswada huo kusomwa kwa mara ya pili.
Alifafanua pia hatua ya chama hicho kwenda Ikulu kumwona rais akisema kuwa rais ni upande wa pili wa Bunge.
Mnyika alisisitiza kuwa Chadema hawatasubiri kwenda mahakamani, ili kupinga sheria hiyo bali watafanya mikutano nchi zima na kueleza ubaya wa sheria hiyo.


“Tutakwenda kwa wananchi tuwaambie ubaya wa sheria hii. Watapiga kura ya hapana, hata kama hatutapata katiba, tutakuwa tumeleta mabadiliko”.
Naye Cheyo alisema mchakato mzima wa kuandikwa kwa katiba mpya umehodhiwa na rais huku wananchi wakizuiwa kutoa maoni yao. “Bunge la kutunga katiba ni Bunge la chama kile kile, limekuwa likiaminiwa na chama hicho hicho.

Tuangalie ‘composition’(wanaounda) ya Bunge, inachukuwa watu gani, vinginevyo tutakuwa hatuwatendei haki wananchi,” alisema Cheyo. Awali asasi mbalimbali ndani ya jamii zikiongozwa na Jukwaa la Katiba Tanzania, zilieleza kutoridhishwa na hatua zilizochukuliwa na serikali katika kuendesha na kusimamia mchakato mzima wa kupitishwa kwa sheria hiyo.
Chanzo:Mwananchi