Kilimanjaro Watakiwa Kutumia Fursa Zilizopo Kujiletea Maendeleo


Mwenyekiti wa Jukwaa la Maendeleo ya mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia alikuwa Makamu wa Rais na Waziri mkuu mstaafu wa Tanzania Cleopa David Msuya akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mkoa wa Kilimanjaro na uendelezaji wa fursa zilizopo kwa maendeleo ya mkoa huo na taifa leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni makamu Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Bw. Arnold Kilewo.

Picha na Aron Msigwa -MAELEZO.

Na. Aron Msigwa -MAELEZO.
Wananchi wa mkoa Kilimanjaro wametakiwa kutumia fursa zilizopo katika mkoa huo zikiwemo mlima Kilimanjaro, uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro kujiletea maendeleo. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Jukwaa la Maendeleo ya mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia alikuwa Makamu wa Rais na Waziri mkuu mstaafu wa Tanzania Cleopa David Msuya amesema wananchi wana jukumu la kushirikiana na serikali katika kutumia fursa zilizopo kujiletea maendeleo.
Amesema kuwa kwa sasa wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za kimaendeleo licha ya kuwepo fursa nyingi za maendeleo huku akisisitiza kuwa iwapo fursa hizo zitaendelea kutumika ipasavyo wananchi watanufaika na umaskini utapungua. Amefafanua kuwa maendeleo ya mkoa huo yapo wazi kutokana na mkoa huo kuwa na maeneo mazuri ya uwekezaji katika shughuli za kilimo, nguvu kazi na miundombinu mizuri ya kurahisisha ufanyaji kazi.

“Ni dhahiri mkoa wa Kilimanjaro ni moja ya mikoa yenye shule nyingi katika Tanzania, hivyo tuna nafasi nzuri ya kupata maendeleo pamoja na mlima Kilimanjaro tulionao ambao ni kivutio kizuri ndani na nje ya nchi yetu” Amesema. Ameongeza kuwa kwa sasa mlima Kilimanjaro bado haujatumika ipasavyo katika kukuongeza pato la Taifa licha ya mlima huo kuwa na fursa nyingi za kuwainua kiuchumi wananchi hasa katika sekta ya utalii.

Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi wa mkoa huo wanaoishi maeneo ya mlima Kilimanjaro kuendelea kutunza mazingira yam lima huo ili uendelelee kuwa kivutio cha watalii na kuongeza pato la taifa. Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa jukwaa hilo Bw.
Arnold Kilewo amefafanua kuwa kwa sasa jukwaa hilo linaandaa utaratibu wa kuwakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo wa mkoa wa Kilimanjaro ili kutathmini na kujadili changamoto mbalimbali za kimaendeleo za mkoa huo na namna ya kuendelea kutumia fursa zilizopo ili kujiletea maendeleo ambapo mgeni rasmi atakuwa Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda

KALAMA NYILAWILA FRANSIC CHEKA USO KWA USO JANUAR 28


Francis Cheka akipiga tizi kiaina

MIAMBA ya masumbwi nchini, bingwa wa Mabara Francis Cheka [SMG] na bingwa wa Dunia Karama Nyilawila [Kapten] wanatarajia kupanda ulingoni Januari 28 mwaka huu kuoneshana umwamba.
Cheka na Nyilawila hawajawahi kutwangana mpambano ambalo limewafanya mashabiki kuhisi kuwa mabondia hao wanaogopana.

Akizungumza Dar es Salaam jana, promota wa pambano hilo Philemon Kyando ‘Don King’ alisema pambano hilo litapigwa katika uwanja wa Jamhuri Morogoro nyumbani kwa Cheka.
Alisema pambano hilo litakuwa la raundi 10 uzito wa kg 72

Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila ‘Super D’ kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi.

Alisema kutakuwa na pambano kati ya Maneno Osward [mtambo wa gongo] na Pasco Ndomba raundi nane uziti wa kg 75, Chaulembo Palasa na Deo Njiku kg 68, Venance Mpoji na Ibrahim Clases kg 63, Anthon Mathias na Juma Afande kg 54 na pambano la mwisho kati ya Hassan Kidebe na Arbert Mbena kg 54 ambapo mapambano hayo yatakuwa ya raundi sita kila moja.

Promota huyo alisema lengo la kumuandalia pambano Nyilawila na Cheka ni kuondoa uvumi kuwa mabondia hao wanaogopana lakini pia ni kuurudisha mchezo wa ngumi katika chati.Chanzo ni http//www.kingkif.blogspot.com

Dk Harrison Mwakyembe Arejea Nchini


NAIBU Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe, amerejea nchini akitokea Hospitali ya Apollo nchini India alikolazwa kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wa ngozi. Dk Mwakymbe aliondoka nchini Oktoba 9 mwaka huu kwenda nchini India baada ya hali yake ya afya kuzorota huku ngozi yake ikionekana kudhoofika.

Baada ya kukaa India kwa takriban miezi miwili, jana saa 7:00 mchana, Dk Mwakyembe aliwasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ndege ya Shirika la Qatar Airways.

Habari zilizolifikia jana mchana zilieleza kuwa baada ya kutua jijini Dar es Salaam, Dk Mwakyembe aliondoka moja kwa moja kuelekea mkoani Mbeya. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana,Msemaji wa Familia na Mbunge wa Lupa,Victor Mwambalaswa alisema, afya ya mbunge huyo wa Kyela, ni nzuri ndio maana ameruhusiwa kutoka hospitali.

“Ni kweli Dk Mwakyembe amerejea nchini salama.Tunamshukuru Mungu, hii inatokana na madaktari waliokuwa wakimpatia matibabu kumpa ruhusa baada ya kuona hali yake ni nzuri na kwamba anaweza kuendelea na majukumu yake kama kawaida,” alifafanua Mwambalaswa na kuongeza:

“Kutokana na hali hiyo, tunaamini kuwa, kurudi kwake nchini, kutaleta matumaini mapya ya afya yake.” Msemaji huyo wa familia alisema, baada ya kurudi, Dk Mwakyembe atapumzika kijijini kwao Kyela ili aweze kujumuika na wanafamilia katika kipindi hiki cha Sikukuu ya Chrismasi na mwaka mpya, kabla ya kuanza kazi rasmi ya ujenzi wa taifa mwakani.

Janbert Kiwia aka JanB Official Website


Hello World, Mambo vipi?Janbert Kiwia, better known in the music entertainment career as JanB a.k.a Bobdee...

Hello World, Mambo vipi?Janbert Kiwia, better known in the music entertainment career as JanB a.k.a Bobdee. Is an upcoming young Tanzanian Swahili rapper, pop singer and song writer aiming to wave Tanzania flag and Promoting Swahili language in music and modeling career to the international level. Currently is doing the music project under Black-curtains records label in Stockholm-Sweden with the super producer Robert Hippolity a.k.a Puzo.
And the first catching audio song for promo ‘‘I Remember Vol.1’’ featured an upcoming Tanzanian RNB singer Obi Elinami which will be available in his free mixtape ”I am JanB” is already out online and doing well in various radio stations in Africa, Europe, America and Australia since the release in November 2011. There are much more to expect from JanB in this music career, indeed.

Apart from music, JanB is a student in Sweden, currently writing his Thesis Project about Energy in Tanzania. Is an independent model for various advertisement jobs and Professionally a Public Relations Practitioner, Solo Consultant and Researcher on Socio-Economic and Environmental arena with a B.A in Public Relations and Advertising from the University of Dar es Salaam in Tanzania and Msc in Sustainable Development from Uppsala University in Sweden.

Why ‘‘I am JanB free mixtape’’?? JanB is trying to be heard and seen first!!

Next week JanB he will release the second song namely ”Playa Haters vol 1.” which is the Swahili version and two weeks after he will release two different songs featured different International artists and Fans will be easily to buy songs and Ringtones via Online store (Itune, Spotify and Amazon).
Please support the New Swahili Rapper ”JanB”. Check out his Official Website and Join.
” I real wanna do something for my life and for my country Tanzania, I’m gonna promote Swahili language via my Swag lyrical music . Yes I can do it, Still I need your support.
If we work as a team Player the world will get to know how good and capable Tanzanians we are. What I need from you now its three easy steps, 1st. Visit my website 2nd. Join and be a member is free 3rd. Start enjoying. Nawapenda sana Fans wangu:)”

JanB