Sio wanaokwenda jela woe wana hatia !


Unaposikia au kuona mtu katoka jela na ugonjwa wa kifua kikuu usishangae sana kwa jinsi ya hii picha inavyokuonyesha hali halisi ya mambo ya huko jela.
Watu wakitoka jela urudi na magonjwa ya ngozi,vifua vikuu na magonjwa mengine ya kuambukiza kutokana na mrundikano wa watu huko jela.tazama pichani jinsi watu wanavyolala..!!mwenye blanketi ndio analo,hasiyenalo hana,utapigwa na baridi mpaka asubuhi.Tukumbuke tu sio wanaokwenda jela wote wenye hatia.

wewe jela pasikie tu !

Wakazi wa Mwanaghati-Kitunda walia na athari za mafuriko


Wakazi wa Mwanaghati-Kitunda walia na athari za mafuriko
Hali ya barabara ya Mwagati-Kitunda si shwari sana kufuatia barabara hiyo kuathiriwa vibaya na mafuriko yaliyotokea hivi karibuni jijini Dar es Salaam na kuathiri miundombinu ya barabara yao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wakzi wa mwagati wameiomba Serikali kupitia Manispaa yao ya Ilala kuwanusuru kwa kufanya ukarabati katika maeneo yote yaliyoathiriwa na mafuriko hayo kwani sasa magari yanapita kwatabu jambo ambalo huenda likiendelea litasababisha kukatika kwa mawasiliano ya daladala katika maeneo hayo.

Blogu ya mrokim. ilishuhudia barabara hizo kama inavyoonekana pichani zikiwa zimeharibika vibaya.

KAMPENI YA “Red Alert” INAYOENDESHWA NA VODACOM TANZANIA YAKUSANYA SHILINGI 6,284,000/= MPAKA SASA


Vodacom Tanzania inawashukuru wote ambao tayari wameshaonesha upendo wao kupitia kampeni ya “Red Alert” na kufanikisha kukusanywa shilingi 6,284,000/= kati ya December 22, hadi December 27, 2011.
Tunapenda kutoa wito wa kuendelea kuchangia Ndugu zetu waliopatwa na janga la mafuriko kwani bado wanahitaji misaada yetu,kwa Kupitia nambari ya Red Alert 15599 mteja anaweza kuchangia shilingi 500 kwa kutuma ujumbe mfupi – SMS wenye neno MAAFA na hakuna ukomo wa ujumbe na kwa njia ya m-pesa mteja anaweza kuchangia kuanzia shilingi 1,000 na zaidi kwenda nambari 155990.
Jinsi ya kuchangia kwa m-pesa
*150*00# kupata orodha ya huduma za m-pesa.
Hatua ya 2: Chagua 4 – Lipa Bili
Hatua ya 3: Weka namba ya kampuni – weka namba 155990
Hatua ya 4: Weka namba ya kumbukumbu – weka namba yako ya simu
Hatua ya 5: Weka kiasi – ni kuanzia Tsh 1,000 na kuendelea
Hatua ya 6: Weka namba yako ya siri
Hatua ya 7: Bonyeza 1 kwa kuhakikisha muamala na tayari utakuwa umeshachangia

BOMOA BOMOA YAANZA JANGWANI NA MABONDENI


Mmoja wa maofisa wa kutoka Manispaa ya Ilala, akiweka alama katika moja ya nyumba eneo la Jangwani

Maofisa wa Manispaa ya Ilala, wakiangalia ramani ya nyumba za Jangwani zilizopigwa kwa setilaiti, kabala ya kuanza kuziweke

Kijana mkazi wa Jangwani, bondeni, Dar es Salaam, akianika balakashia jana, zilizokuwa zimelowa wakati wa mafuriko yaliyolikumba Jiji la Dar es Salaam

.Chanzo:http://www.richard-mwaikenda.blogspot.com/

Sengondo Mvungi:Vyombo Vya Habari Viliandika Visivyo Uamuzi Wa Mahakama Kuu Kuhusu Shauri la Mbunge wa Kigoma Kusini(NCCR-MAGEUZI),David Kafulila Alilolipeleka Mahakamani


Mkuu wa Idara ya Katiba, Sheria na Haki za Binadamu wa NCCR-Mageuzi, Sengondo Mvungi akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam, ambapo alilalamikia vyombo vya habari kwamba viliandika visivyo uamuzi wa Mahakama Kuu,Kanda ya Dar es Salaam, kuhusu shauri la Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila alilolipeleka mahakamani kuomba zuio la hatua zilizochukuliwa dhidi yake na chama hicho. Kushoto ni Martine Juju, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho.
Picha na Habari na Richard Mwaikenda.