Day / December 19, 2011
Mhe. Zitto Kabwe Atoa Kauli Juu Ya Kufukuzwa Kwa Mheshimiwa David Kafulila NCCR-MAGEUZI
—
Leo(Jana) kwa masikitiko makubwa sana nimesoma kwenye vyombo vya habari kwamba ndugu David Kafulila kavuliwa uanachama wa chama chake. Kwa hatua hii David anakuwa amepoteza Ubunge wa jimbo la Kigoma Kusini licha ya kwamba alichaguliwa na wananchi bila kujali vyama (NCCR-M wanachama wake huko Kigoma Kusini hawafiki hata asilimia 10 ya wapiga kura wote). Haya ndio madhara ya Katiba ya sasa. Katakana na historia ya kisiasa baadhi ya watu wanajaribu kunihusisha na matatizo ya chama cha NCCR-M. Napenda kuweka wazi kwamba sihusiki kwa namna yeyote ile na migogoro ya chama kile.
Ninaomba nisihusishwe na mambo yasiyonihusu. Ni dhahiri kwamba kuvuliwa uanachama kwa David ni jaribio kubwa kwa mfumo wetu wa demokrasia kama ilivyokuwa huko nyuma wakati kina Erasto Tumbo walipovuliwa uanachama wa chama chao cha UDP. Ninaamini NCCR-M watamaliza matatizo yao kwa mujibu wa katiba ya chama chao na ndugu David Kafulila atazikabili changamoto hizi kama kiongozi kijana wa kisiasa na kuona hii kama fursa badala ya kukata tamaa. Ifahamike wazi kabisa kwamba David ni mtu huru mwenye mawazo yake na maamuzi yake. Kwamba sisi ni marafiki wa karibu na kwamba tunatoka mkoa mmoja haina maana kwamba lolote afanyalo ama nimemtuma au ninahusika.
Ninaheshimu misimamo yake na siku zote huwa nipo upande wa anayeonewa, kudhulumiwa na mnyonge. Msimamo huu wa msingi usiwape watu nafasi ya kunihusisha na mambo ya chama dhaifu kisicho na dira kama NCCR-M.
Kafulila akumbuke kwamba hakufukuzwa CHADEMA, alijiondoa mwenyewe. Milango yetu ipo wazi kwa mujibu wa Katiba, Kanuni na taratibu za chama chetu.
Ndg. Kabwe Zuberi Zitto, Mb
18 Disemba 2011
VODACOM TANZANIA YAZINDUA DUKA JIPYA JIJINI DAR
VODACOM TANZANIA YAZINDUA DUKA JIPYA JIJINI DAR
FAINALI ZA MASHINDANO YA MITUMBWI ZANOGA
Washiriki wa shindano la Mitumbwi Balimi Extra Lager wakiwa tayari kuondoka wakisubili filimbi kupulizwa
Washiriki wa shindano la Mitumbwi Balimi Extra Lager wakiondoka baada ya filimbi kupulizwa.
Washiriki wa shindano la Mitumbwi Balimi Extra Lager wakiwa katikati ya maji wakati a shindano hilo .
Wakazi wa Jijini Mwanza wakishuhudia mashindano ya Mitumbi ya Balimi Extra Lager Mwaloni Jijini Mwanza mwishoni mwa wiki
Mkuu Wa Mkoa Wa Rukwa Mhe. Eng. Stella Martin Manyanya (MB) Ameliomba Shirika la Tanesco Wasikate Umeme Mkoa Rukwa Kipindi Hiki Cha Maandalizi Ya Sensa Ya Watu
Mkuu Wa Mkoa Wa Rukwa Mhe. Eng. Stella Martin Manyanya (MB) Ameliomba Shirika la Tanesco Wasikate Umeme Mkoa Rukwa Kipindi Hiki Cha Maandalizi Ya Sensa Ya Watu
MADA MAUGO AMTWANGA SELEMANI SAIDI KWA KO RAUNDI YA TATU
MADA MAUGO AMTWANGA SELEMANI SAIDI KWA KO RAUNDI YA TATU
RAIS JAKAYA KIKWETE AWAAPISHA MABALOZI WAPYA IKULU DAR LEO
Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha, Phillip Marmo, kuwa Balozi wa China, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha mabalozi wapya iliyofanyika leo mchana Desemba 19, Ikulu Dar es Salaam. Mabalozi wapya waliofika Ikulu Dar es Salaam leo kwa ajili ya kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete, wakisubiri kuapishwa. Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha, Dkt. Batilda Buriani, kuwa Balozi wa Kenya, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha mabalozi wapya iliyofanyika leo mchana Desemba 19, Ikulu Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha, Dkt. Deodorus Kamala, kuwa Balozi wa Ubelgiji, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha mabalozi wapya iliyofanyika leo mchana Desemba 19, Ikulu Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha, Ally A. Saleh, kuwa Balozi wa Oman, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha mabalozi wapya iliyofanyika leo mchana Desemba 19, Ikulu Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha, Shamim Nyanduga, kuwa Balozi wa Msumbiji, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha mabalozi wapya iliyofanyika leo mchana Desemba 19, Ikulu Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto), Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (kulia) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, wakizungumza jambo, baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kuwaapisha mabalozi wapya iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam leo, Desemba 19. Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wapya baada ya kuapishwa rasmi leo Ikulu Dar es Salaam.
Samim Nyanduga, akipongezwa na Mumewe, baada ya kuapishwa rasmi kuwa Balozi wa Msumbiji, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam leo. Nyuma yao ni wanafamilia wa Familia hiyo.
Picha Zote na Muhidin Sufiani-OMR